Malenga Makali ni jina la kata ya tarafa ya Ismani, Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,917 waishio humo. [1]

Vijiji vyake ni kama vileː Usolanga, Iguluba, Makadupa, Mkulula na Nyakavangala.

Ni eneo maarufu kwa kilimo hasa cha mahindi, ingawa ardhi imechoka kutokana na matumizi makubwa, hasa katika miaka ya 1950 na 1960, Ismani peke yake ilipokuwa inaweza kuzalisha kuliko Tanzania nzima.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki na Walutheri.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania  

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malenga Makali kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.