Mapaliko na wenzake

Mapaliko na wenzake Baso, Fortunio, Paulo, Fortunata, Viktorino, Viktori, Eremio, Kredula, Ereda, Donato, Firmo, Venusto, Frukto, Julia, Marziale na Aristone (walifariki 250 hivi) walikuwa Wakristo wa Afrika Kaskazini (Tunisia ya leo) katika karne ya 3.

Wakati wa dhuluma ya kaisari Decius, wote walikubali kuteswa na hatimaye kuuawa kwa ajili ya imani yao, wengi wao kwa kuachwa bila chakula gerezani hadi kufa.

Askofu wa Karthago Sipriani mfiadini aliandika juu yao.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa hasa tarehe 19 Aprili[1][2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.