Sipriani (kwa Kilatini: Thascius Caecilius Cyprianus; 210 hivi - 14 Septemba 258) alikuwa askofu wa Karthago na mwandishi muhimu kati ya Mababu wa Kanisa, ambaye vitabu vyake vya Kilatini viko hadi leo [1].

Picha takatifu ya Mt. Sipriani.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Septemba[2] pamoja na Papa Kornelio[3] kwa kuwa waliungana kushuhudia upendo kwa ukweli ule ambao haukubali kuyumbishwa na ambao wao waliuungama mbele ya Kanisa la Mungu na ulimwengu nyakati za dhuluma [4].

Maisha

hariri

Alizaliwa mwanzoni mwa karne ya 3 katika eneo la Afrika kaskazini, labda huko Karthago, alipopata elimu na kuwa mhubiri maarufu.

Baada ya kuongokea Ukristo kwa msaada wa padri Sesili (245), alipata mapema kuwa shemasi, padri akachaguliwa kuwa askofu mwaka 249 na hatimaye akafia dini.

Maandishi yake

hariri

Yanapatikana katika magombo 3 na 4 ya Patrologia Latina.

Kitabu chake muhimu zaidi ni "De unitate ecclesiae" (Umoja wa Kanisa). Humo aliandika: "Hawezi kuwa na Mungu kama Baba yule asiye na Kanisa kama mama; . . . asiyekusanya katika Kanisa analitawanya Kanisa la Kristo" (vi.); "Hakuna nyumba nyingine kwa waamini isipokuwa Kanisa pekee" (ix.).

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.