Margarita Bourgeoys
Margerita Bourgeoys, CND (17 Aprili 1620 - 12 Januari 1700[1]), alikuwa mtawa wa Ufaransa na mwanzilishi wa Shirika La Notre Dame wa Montreal katika koloni la New France, ambayo sasa ni sehemu ya Québec, Kanada.
Alitangazwa rasmi mwenyeheri na Papa Pius XII tarehe 12 Novemba 1950, halafu mtakatifu na Papa Yohane Paulo II 31 Oktoba 1982.
Maisha
haririMzaliwa wa Troyes, alisafiri kwenda Fort Ville-Marie (sasa Montreal) mwaka 1653, ambapo aliendeleza kwa bidii kubwa mabinti wa wasomi, maskini, na Waindio hadi muda mfupi kabla ya kifo chake[3].
Kabla Bourgeoys hajapata kutambuliwa mnamo 1982 kama mtakatifu katika Kanisa Katoliki, watu wengi tayari waliamini kuwa alikuwa na sifa hiyo kwa jinsi alivyosaidia kwa kila njia wahamiaji. Siku iliyofuatia kifo chake, kuhani aliandika, "Ikiwa watakatifu wangetangazwa kama zamani na sauti ya watu na ya wachungaji, kesho tungekuwa tunasema Misa ya Mtakatifu Margerita wa Kanada." Helene Bernier aliandika, "Pongezi zake mara nyingi zilikuwa zimeshatangazwa miaka 250 kabla ya kutangazwa kwake mtakatifu."
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Marguerite Bourgeoys (1620-1700) - biography, Vatican News Service
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |