Marko wa Efeso (jina la awali: Manuel Eugenikos; Konstantinopoli, 1392 - Konstantinopoli, 23 Juni 1444) alikuwa mmonaki, mshairi[1] na mwanateolojia wa Kiorthodoksi kutoka Dola la Bizanti na askofu mkuu wa Efeso.

Picha takatifu ya Mt. Marko wa Efeso.

Alipata umaarufu kwa kushiriki katika Mtaguso wa Ferrara-Florence (14381439) na kushika msimamo mkali zaidi dhidi ya madai ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya muungano.

Mwaka 1734 alitangazwa na Patriarki Serafim I wa Konstantinopoli pamoja na sinodi yake kuwa mtakatifu.

Aliacha maandishi mengi, yakiwemo ya tenzi, vitabu vya teolojia, anthropolojia n.k.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Mineva, Evelina (2000). The Hymnographic Opus of Mark Eugenikos (in Greek). Athens. 

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.