Marvel Cooke

Mwanamke wa kwanza Mwafrika kufanya kazi katika gazeti la kawaida linalomilikiwa na wazungu (1903-2000)


Marvel Jackson Cooke (Aprili 4, 1903Novemba 29, 2000) alikuwa mwandishi wa habari na machaapisho tofauti, pia alikuwa mpigania haki za binadamu kutoka nchini Marekani. Marvel Jackson Cooke ndiye aliyekuwa mwanamke Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kufanya kazi katika kampuni ya gazeti inayomikikiwa na Mzungu.

Marvel Cooke
Faili:Marvel Cooke.jpg
Amezaliwa Marvel Cooke
Aprili 4 1903
Mankato
Nchi Marekani
Kazi yake mwandishi wa habari
Cheo Mwandishi

Maisha ya Awali na Elimu

hariri

Marvel Jackson ni mtoto wa kwanza mwenye asili ya kiafrika aliyezaliwa Mankato, Minnesota.[1][2] Wazazi wake walikuwa ni Madison Jackson na Amy Wood Jackson.[2] Baba yake ni mhitimu wa sheria katika Chuo kikuu jimbo la Ohio na kuwa mwanachama wa Dakota Bar ya kusini, ila hakuweza kupata kazi kama mwanasheria mweusi. Hapo awali mama yake aliwahi kuishi wanapohifadhiwa wazawa kama mpishi na mwalimu wa mapishi. Amy Wood Jackson aliacha kazi hifadhini kusini mwa Dakota baada ya kushuhudia unyanyaswaji wa wazawa wa Marekani eneo lile. Baada ya kuacha kazi yake ya mapishi, ndipo alipoamua kuwa mama wa nyumbani na kuamua kuwatunza watoto wake wakiwemo Marvel na dada zake watatu kwa muda wote.

Marvel alipitia madhara ya ubaguzi wa rangi akiwa na umri mdogo sana. Alilelewa maisha ya daraja la juu, jirani kabisa na waishipo Wazungu pale Minneapolis pale familia yake ilipohamia mnamo mwaka 1907. Baada ya manunuzi ya nyumba yao ya kwanza, wakazi waliandamana baraza la Jackson kupinga tukio la watu weusi kuishi karibu na jamii zao. Shule na Taasisi za elimu kipindi hicho kilikuwa bado hakina utengano, ila baada ya familia ya Marvel kuhamia na watoto kuanza shule, matengano yakaanza. Pia aliweza kumsikia mwalimu wake kipenzi akitumia lugha ya kibaguzi pindi akiwa katika madarasa ya awali na rafiki yake kipenzi alikuja kumtenga pindi alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba sababu ya kuwa mweusi. Mnamo mwaka 1921, Marvel alijiunga katika chuo kikuu Minnesota.

Ni wanawake wanne tu ndio waliofanikiwa kujiunga chuo kikuu pamoja na yeye, katika jumla ya wanafunzi 20,000. Aliweza kuwa mwasisi wa Alpha Kappa sura ya Alpha chuoni, alipohudhuria. Mwanzoni mwa kujiunga na Chuo, Marvel aliweza kufaulu mitihani ya serikali na kuwa mkalimani wa Lugha ya Hispaniola na kuwa katika kitengo cha Vita.

Licha ya matokeo yake ilimwezesha kupata kazi, tajiri yake alimpa kazi kama karani kwa kumdanganya kwa kumwambia kitengo cha ukalimani bado hakijaanzishwa rasmi. Baadae Cooke aliweza pata ukweli kuwa kitengo cha ukalimani ulianzishwa ila waliajiri wanawake wa kizungu pekee; ndipo alipowasiliana na Mtawala wa jimbo, Bwana Henrik Shipstead, aliyeweza kumsadia kumpatia kazi katika kitengo cha ukalimani.

Mnamo mwaka 1925, Marvel aliweza hitimu Chuo kikuu cha Minnesota na kufanikiwa kupata shahada ya kiingereza, akiwa tu na umri wa miaka 22 tu.

Cooke aliweza kupata kazi kama msaidizi wa W. E. B. Du Bois, mhariri wa gazeti la NAACP The Crisis, na mnamo mwaka 1926 alikwenda katika jimbo la New York, akiwa na makazi Harlem, wakati wa vuguvugu la kisiasa jinini Harlem. Kabla ya kushughulika katika vuguvugu hiyo, Before working at The Crisis, hakuwa amesomea uandishi wa habari wala kufanya kazi katika taasisi ya gazeti yeyote. Uwezo na kipaji chake cha uandishi kiliweza vumbuliwa na Du Bois, aliyempa majukumu kuandika safu katika gazeti, ambapo mukthasari wake ulihusisha pingamizi ya kazi ya waandishi wakongwe na mashuhuri wa siku kama vile, Langston Hughes, Zora Neale Hurston na Dorothy Parker. Kwa kuongezea katika safu la gazeti, lililoitwa "In the Magazines," Cooke aliandika gazetini. Akiwa chini ya uangalizi wa Du Bois, aliweza kuwa karibu na waandishi na wasanii mashuhuri akiwemo Paul Robeson, Countee Cullen, Elizabeth Catlett, Richard Wright, Langston Hughes, Arna Bontemps na James Weldon Johnson. Alikuja kuvunja uhusiano wake na Roy Wilkins ( ambapo baadae alikuja kuwa kiongozi wa NAACP) kwa kumuona kuwa msiri sana.

Harakati

hariri

Mnamo mwaka 1927, alikwenda fanya kazi katika shirika la New Yoek Amsterdam, ambapo ailikuwa mtangazaji wa habari mwanamke wa kwanza mnamo wakiwa na miaka ya 40 katika historia.] Mnamo mwaka 1929, aliweza kuolewa na Mjamaika Cecil Cooke – mhitimu wa chuo kikuu cha Columbia, aliekuwa mwanariadha mashuhuri mbio za maili chache walipokutana walidumu kwenye ndoa mpaka kifo kilipowatenganisha mnamo mwaka 1978. Baada ya ndoa, walienda kuishi Greenboro, Karolina Kaskazini pale ambapo Marvel alifundisha historia, Kiingereza na Kilatino katika madarasa ya juu idara ya kilimo na ufundi katika chuo cha North Karolina. chuo cha Karolina Kaskazini. Baada ya kurudi New York na shirika la habari Amsterdam News mnamo mwaka 1931, alisaidia kuanzishwa kwa sura ya kwanza katika gazeti hilo na kilihusika katika mgomo uliodumu kwa takribani miezi 11 na wahariri hawakuruhusiwa ndani, mpaka mgomo unapokuja kuiha mnamo msimu wa sikukuu za Krismasi mwaka 1934. Cooke hakupenda hadithi za kiuhalifu alizopewa na taasisi ya habari, na kuona isiyokuwa na ladha kufanya kazi hiyo na kupendekeza kuongeza nakala katika gazeti hilo kwa sanaa, alitumia gharama zake binafsikwenda kuchukua taarifa katika maonesho ya kumbukumbu ya Lincolin mnamo mwaka 1939. Pia aliweza kutoa taarifa alizoona kuwa za uhakika kuhusu jamii ya watu weusi na kutumia kurasa za mbele kuonesha matatizo yanyokumba wana maonyesho wa Apollo disliked the crime stories she was na kuelezea uhalifu mjini Harlem. Cooke eventually left the paper for good in 1940.Hakupenda vichwa vya habari vyenye hisia kama She disliked a sensational headline ("Mpenzi alieuawa, Alilala na Mwili") na maandiko mengine mengi yenye hisia. Akiwa anafanya kazi katika shirika la habari la Amsterdam, Cooke alimhoji mwanmke tajiri sana eneo kwenye jumba moja. Hakuruhusiwa kuingia kupitia mlango wa mbele kutokana na na rangi ya ngozi yake, hivyo alibidi ampigie mhojiwa na kuahirisha mahojiano. Mhojiwa ilibidi amshurutishe mmiliki wa jengo hilo na kumruhusu Cooke kupitia mlangoni.

Mnamo mwaka 1942 mpaka 1947, Cooke alifanya kazi katika shirika la People's voice ( Chapisho la kila wiki linalomilikiwa na Adam Clayto Powel) kama mhariri msaidizi. Habari za uhalifu kutoka kwenye kituo cha habari cha People'Crime kilikuwa penzi kwa Cooke ukilinganisha na kazi alizowahi fanya awali katika habari. Gazeti hilo lilishindwa vibaya kibiashara mnamo mwaka 1947. Mnamo mwaka 1950, aliajiriwa katika Gazeti la the New York Paper, "The daily Compass, na kuwa Mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke kufanya kazi kama mwandishi katika gazeti linalomilikiwa na Mzungu; wakati huo kulikuwa na waandishi weusi wawili pekee pale, akiambatana na Richard Carter kazi zake za mwanzo, mwanzoni mwa mwezi April 16, ilikuwa kazi: Streetwalker" ambayo ilikuwa ya historia na kuhusisha ukahaba unaofanyika katika eneo hilo, pia aliandika nakala inayosomeka kama, kutoka pipi mpaka madawa.", Mamlaka ya Jiji la New York walianza mchakato wa kupunguza utumiaji wa dawa za kulevya baada ya uchapishwaji wa jarida la “From Candy to Heroin”

Marejeo

hariri
  1. Keith A. P. Sandiford, A Black Studies Primer: Heroes and Heroines of the African Diaspora, Hansib Publications, 2008, p. 134.
  2. 2.0 2.1 Diggs-Brown, Barbara; Streitmatter, Rodger (Julai 31, 1992). "Marvel Cooke: An African-American Woman Journalist Who Agitated for Racial Reform". Afro-Americans in New York Life and History. 16 (2). Kigezo:ProQuest.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marvel Cooke kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.