Ukoo

kundi la watu wamoja na ujamaa halisi
(Elekezwa kutoka Mbari)

Ukoo ni chanzo na muunganiko wa familia kadhaa zenye asili moja[1]. Mara nyingi huwa na utamaduni na lugha moja. Ukoo huundwa na vizazi mbalimbali ambapo mila na desturi zao huendelezwa na kuhifadhiwa kwa faida ya vizazi vya baadae. Mfano mmojawapo ni ukoo wa Mkwawa uitwao ukoo wa Mwamuyinga[2].

Ukoo wa Wahehe mkoani Iringa mwanzoni mwa karne ya 20.

Katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, ukoo ni kitengo cha shirika la kijamii. Ni muundo wa zamani sana wa jamii katika eneo hilo, zaidi ya familia na kizazi. Muundo huo unapatikana katika Rwanda ya sasa, Burundi, Tanzania na Uganda.

Watu wa eneo hilo hutumia maneno tofautitofauti ya kiasili kuelezea dhana hiyo: ubwoko nchini Rwanda, umuryango nchini Burundi, ruganda katika falme za Bunyoro na Buhaya, igise huko Buha, ishanja huko Buhavu na ebika huko Buganda.

Uanachama wa ukoo ni dhana huru, yenye uwiano na nasaba, iliyojikita zaidi katika utamaduni na imani binafsi kuliko ushahidi halisi.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukoo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.