Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo

Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo (kwa Kiingereza: International Fund for Agricultural Development; kifupi: IFAD) ni taasisi ya kifedha ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa yenye jukumu la kushughulikia umaskini na njaa katika nchi zinazoendelea.

Historia hariri

IFAD ilianziswa kama taasisi ya kifedha mnamo mwaka 1977 kupitia azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa 32/107 la tarehe 30 Disemba 1977) kama moja ya matokeo ya Mkutano wa dunia juu ya chakula wa mwaka 1974.

Makao makuu ya taasisi hiyo yapo mjini Roma, Italia, na ni mshirika wa mkutano wa Umoja wa Mataifa ya maendeleo (kwa Kiingereza: United Nations Development Group). [1]

Rais wa IFAD ni Gilbert F. Hounbo kutoka Togo, ambaye alichaguliwa kwa miaka minne tangu 2017.

Tanbihi hariri

  1. UNDG Members. Jalada kutoka ya awali juu ya 11 May 2011. Iliwekwa mnamo 2012-05-15.

Viungo vya nje hariri