Vijiwimbi[1] (pia: mikrowevu au wimbi mikro; kutoka Kiingereza microwave) ni aina ya mawimbi ya sumakuumeme inayofanana na mawimbi ya redio, lakini masafa ya mawimbi yake ni mafupi zaidi. Haionekani kwa macho ya binadamu. Masafa ya vijiwimbi yako kati ya mita 1 hadi milimita 1; marudio ni kati ya 300 MHz (0.3 GHz) na 300 GHz.

Masafa ya vijiwimbi yako kati ya mawimbi ya redio na infraredi katika spektra ya mawimbi ya sumaukumeme

Matumizi ya vijiwimbi

Katika maisha ya kila siku vijiwimbi vinajulikana zaidi kutokana na matumizi yake katika majiko ya kupashia moto chakula.

Lakini zinatumiwa katika teknolojia ya mitambo mingi pamoja na rada, mawasiliano ya simu za upepo, bluetooth na waifai. Kuna uchunguzi kwa matumizi yake ya kijeshi, yaani kama silaha.

Mikrowevu kama jiko

Jiko la mikrowevu linafanya kazi kwa sababu mawimbi yake yanaathri molekuli ya maji ndani yake kujipanga kama sumaku ndogo. Baadaye mwelekeo unabadilishwa kinyume. Kwa njia hiyo molekuli za maji ndani ya jiko zinachezacheza. Mwendo huu unaongeza kiwango cha joto ya maji na kwa njia hiyo ya kila kitu chenye unyevu ndani yake kilichopo ndani ya jiko la mikrowevu.

Kwa njia hiyo vyakula vyenye maji ndani yake vinaweza kupashwa moto haraka sana. Ila tu matoleo si mazuri kwa vyakula vikavu sana.

Vilevile vitu vilivyojengwa kwa molekuli zisizokubali kuathiriwa kisumaku hazipashwi moto. Kumbe aina za plastiki zinaweza kukaa kwenye mikrowevu bila matata yaani chakula kinakuwa cha moto lakini sahani ya plastiki ya kufaa inabaki baridi.

Marejeo

  1. Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: TUKI. 1990. uk. 101. ISBN 9976911092.

Viungo vya Nje

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kijiwimbi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.