Akili ya binadamu

(Elekezwa kutoka Mind)

Akili ya binadamu (kwa Kiingereza "mind"[3]) ni kipawa kinachowezesha kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo. Ni ufahamu uliomo katika ubongo hasa wa binadamu, unaomwezesha hata kutofautisha jambo kwa wema na ubaya wake upande wa maadili na hatimaye kumuongoza katika kufanya maamuzi kwa kutumia hiari yake[4].

Ramani ya ubongo[1] ikionyesha sehemu zake zinavyohusika na kazi tofautitofauti.
Mchoro wa René Descartes[2].

Dhana kuhusu asili ya akili ya binadamu zinatofautiana, vilevile na maelezo mengine mengi, kulingana na dini, falsafa na sayansi[5] husika.

Jambo mojawapo la msingi ni kuelewa kama akili hiyo ya pekee inategemea tu ubongo uliokua sana katika binadamu kuliko katika spishi nyingine au kuna athari kubwa ya roho ndani yake. Hii ni kwa sababu watu walichoweza kufanya hakifanani kabisa na wanyama walichofanya, hata wale walio na ujirani naye kibiolojia kama sokwe.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Oliver Elbs, Neuro-Esthetics: Mapological foundations and applications (Map 2003), (Munich 2005)
  2. Descartes, R. (1641) Meditations on First Philosophy, in The Philosophical Writings of René Descartes, trans. by J. Cottingham, R. Stoothoff and D. Murdoch, Cambridge: Cambridge University Press, 1984, vol. 2, pp. 1–62.
  3. "mind – definition of mind in English | Oxford Dictionaries". Oxford Dictionaries | English. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-19. Iliwekwa mnamo 2017-05-08.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  4. Başar, Erol (2010). Brain body mind oscillations in scope of uncertainty principle. New York: Springer. uk. 5. ISBN 978-1441961365. 
  5. Harnad, S.R., Steklis, H.D., & Lancaster, J.E. (1976). "Origins and evolution of language and speech". Annals of the New York Academy of Sciences 280 (1): 1–2. Bibcode:1976NYASA.280....1H. doi:10.1111/j.1749-6632.1976.tb25462.x. 

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akili ya binadamu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.