Swila-bahari
Swila-bahari | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mkiadau (Hydrophis platurus)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Jenasi 10:
|
Swila-bahari ni nyoka wenye sumu wa jenasi mbalimbali wa nusufamilia Hydrophiinae katika familia Elapidae. Kama jina lao linaonyesha, nyoka hawa wanaishi baharini. Spishi ya Afrika ya Mashariki huitwa mkiadau pia.
Takriban spishi zote zinafika urefu wa m 1.2-1.5, lakini kuna spishi ndefu zaidi. Hydrophis spiralis anaweza kuwa m 3. Mwili ni bapa wenye mkia kama kasia. Macho yao ni madogo na matundu ya pua yapo juu kwa sababu lazima waweke pua juu ya maji ili kupumua. Spishi nyingine zina rangi moja, kama kijivu au kahawia, lakini nyingine zina miviringo au mabaka meusi au buluu.
Swila-bahari huishi baharini tu lakini spishi za jenasi Laticauda zinapenda kupanda juu ya ufuko mara kwa mara. Hula pweza wadogo, gegereka na samaki.
Sumu ya swila-bahari ni kali sana, lakini spishi nyingi hazing'ati sana na watu wachache tu wanakufa kwa sababu ya nyoka hawa kila mwaka. Hata hivyo mkiadau anaweza kuingiza sumu ya kutosha kwa kuua mtu kwa sababu nyoka huyu hutumia sumu yake ili kujihami.
Spishi ya Afrika
hariri- Hydrophis platurus, Mkiadau au Swila-bahari Tumbo-njano (Yellow-bellied sea snake)
Jenasi za Asia na Australia
hariri- Aipysurus: spishi 9 (Aipysurus)
- Emydocephalus: spishi 3 (Emydocephalus)
- Ephalophis: spishi 1 (Ephalophis)
- Hydrelaps: spishi 1 (Hydrelaps)
- Hydrophis: spishi 47 (Hydrophis)
- Kolpophis: spishi 1 (Kolpophis)
- Laticauda: spishi 8 (Laticauda)
- Parahydrophis: spishi 1 (Parahydrophis)
- Parapistocalamus: spishi 1 (Parapistocalamus)
- Thalassophis: spishi 1 (Thalassophis)
Picha
hariri-
Olive seasnake (Aipysurus laevis)
-
Turtlehead sea snake (Emydocephalus ijimae)
-
Slender-necked sea snake (Hydrophis melanocephalus)
-
Yellow-lipped sea krait (Laticauda colubrina)
-
Anomalous sea snake (Thalassophis anomalus)
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Swila-bahari kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |