Mlango wa Malakka
Mlango wa Malakka ni mlangobahari kati ya Malaysia na kisiwa cha Sumatra (Indonesia) wenye urefu wa km 930. Unaunganisha Bahari Hindi na Bahari ya Uchina ambayo ni bahari ya kando ya Pasifiki.
Bandari muhimu zaidi ni Malakka (Malaysia) na Singapur.
Ni kati ya njia za bahari zinazotumiwa zaidi duniani. Kila siku meli 2,000 zinapitia humo, kwa jumla 20 - 25.5% ya biashara yote ya baharini inategemea mlangobahari huo.