Msimbo bandia
Makala hii, au sehemu za makala hii, inahitaji vyanzo au marejeo yoyote. Tafadhali saidia kuboresha makala hii kwa kuweka vyanzo vya kuaminika. Habari zisizowekewa vyanzo zinaweza kuwekewa alama na kuondolewa. |
Msimbo bandia (kwa Kiingereza: Pseudocode) ni njia isiyo rasmi ya kuandika msimbo chanzo usiyozingatia sheria au muundo rasmi wa lugha ya programu au teknolojia itakayotumika. Hutumika kuandaa muhtasari au rasimu ya haraka haraka ya programu. Msimbo bandia huonyesha muhtasari wa mtiririko wote wa programu bila kuelezea taarifa zote za msingi. Wabunifu wa mifumo hutumia misimbo bandia ili wasanidi programu waweze kuelewa mahitaji ya mradi wa programu na kuandika misimbo kama inavyotakiwa.
Msimbo bandia ni njia rahisi kwa binadamu kuonyesha mantiki ya programu kabla ya kuandika msimbo chanzo wenyewe. Hutumia lugha ya kawaida na sintaksi mithiri ya lugha za programu kuonyesha hatua kwa hatua mtiririko mzima wa programu. Msimbo bandia hauchakatwi na kompyuta kwasababu sio programu ila hutumika kama ramani itakayoongoza uandishi wa mwisho wa msimbo chanzo [1].
Matumizi
haririKwenye vitabu vya kiada na machapisho ya kisayansi yanayohusiana na sayansi ya kompyuta na hisabati, msimbo bandia hutumika kuelezea utendaji kazi wa algoriti ili wasanidi programu waweze kuielewa hata kama hawatumii lugha ya programu moja. Kiwango cha taarifa kwenye msimbo bandia kwa baadhi ya kesi huweza kufikia kile cha lugha ya programu.
Msanidi programu anayetaka kutumia algoriti fulani haswa ile ngeni kwake, huanza kwa kuandika msimbo bandia kisha hufasiri huo msimbo bandia kwenda kwenye lugha ya programu anayoitumia. Kabla ya kuanza mradi wa programu, msanidi programu anaweza anza na msimbo bandia kabla ya kuanza rasmi uandishi wa msimbo chanzo.
Sintaksia
haririKwa kawaida, msimbo bandia sio lazima ufate muundo au sintaksi ya lugha yoyote ile, hakuna fomu moja inayokubalika na wote ya kuandika misimbo bandia. Baadhi ya waandishi hukopa mtindo na sintaksi kutoka kwenye lugha za programu kama C, C++ , Java, au Python.
Kulingana na maamuzi ya mwandishi, misimbo bandia hutofautiana kwenye mtindo, kwa baadhi unaweza fanana na lugha ya programu na kwa wengine huwa ni maelezo mafupi tu ya utendaji kazi wa programu
Mtindo wa Pascal: procedure fizzbuzz;
for i := 1 to 100 do
print_number := true;
if i is divisible by 3 then begin
print "Fizz";
print_number := neutral;
end;
if i is divisible by 5 then begin
print "Buzz";
print_number := false;
end;
if print_number, print i;
print a newline;
end
|
Mtindo wa C: fizzbuzz() {
for (i = 1; i <= 100; i++) {
print_number = true;
if (i is divisible by 3) {
print "Fizz";
print_number = false;
}
if (i is divisible by 5) {
print "Buzz";
print_number = false;
}
if (print_number) print i;
print a newline;
}
}
|
Mtindo wa Python: def fizzbuzz():
for i in range(1,101):
print_number = true
if i is divisible by 3:
print "Fizz"
print_number = false
if i is divisible by 5:
print "Buzz"
print_number = false
if print_number: print i
print a newline
|
Marejeo
hariri- ↑ "What is Pseudocode? Definition of Pseudocode, Pseudocode Meaning". The Economic Times (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-05.