Mtaguso wa Vienne

Mtaguso wa Vienne (1311-1312) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano.

Kanisa kuu la Vienne (Ufaransa) ambamo mtaguso ulifanyika.

Mazingira ya kihistoriaEdit

Mtaguso huu ulifanyika Vienne (Ufaransa) baada ya mashindano kati ya Papa Boniface VIII (1294-1303) na mfalme wa Ufaransa Filipo IV.

Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake, Papa Klementi V (1305-1314), alikubali kubaki Avignon (leo nchini Ufaransa) karibu na himaya ya mfalme huyo. Mapapa walibaki huko hadi mwaka 1377, waliporudi Roma.

Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati Regnans in excelsis (12 Agosti 1308) ili kuitisha mtaguso mkuu huko Vienne tarehe 1 Novemba 1310, kwa lengo la kujadili mada 4:

  1. suala la Wahekalu;
  2. vita vya msalaba;
  3. hali ya imani na Kanisa kwa jumla;
  4. urekebisho wa Kanisa.

Mtaguso wenyewe na maamuzi yakeEdit

Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe 16 Oktoba 1311, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.

Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.

Suala la WahekaluEdit

Mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila ya kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.

Suala la Vita vya msalabaEdit

Mtaguso uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza zaka kwa miaka sita, lakini mfalme alijitwalia hizo pesa bila ya kutekeleza ahadi yake ya kuongoza vita hivyo.

Suala la imaniEdit

Mtaguso ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya watawa, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.

Suala la urekebishoEdit

Mtaguso ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na serikali za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya maaskofu, maparoko na watawa.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa Vienne kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.