Chari

(Elekezwa kutoka Mto Chari)

Chari (Shari) ni mto mkubwa unaoishia katika Ziwa Chad. Unaanza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ukielekea kaskazini na kuingia nchi ya Chad. Baada ya kupita mji mkuu N'Djamena mto uunaunda mpaka na Kamerun halafu unaishia katika Ziwa Chad.

Mto wa Chari
Mto Chari
Mdomo Ziwa Chad
Nchi Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Kamerun
Urefu 1,200 km
Kimo cha chanzo 500 - 600 m
Mkondo ??
Eneo la beseni 669,706 km²

Chari inatiririsha 90% ya maji yote ya kuingia ziwa Chad.

Idadi kubwa ya wakazi wa nchi ya Chad wanaishi karibu na mto, wakiwa pamoja na wale wa mji mkuu.

Wavuvi kwenye mto Chari.

Watu wanapata maisha yao mtoni kwa kilimo na uvuvi, hasa wa samaki aina ya sangara.

Tawimto muhimu zaidi ni mto Logone, mengine ni Bahr Salamat, Bahr Sarh, Bahr Aouk na Bahr Keïta.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chari kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.