Frati
Mto Frati (Kigiriki: Ευφράτης euphrátēs; Kiakkadi: Pu-rat-tu; Kiebrania: פְּרָת Pĕrāth; Kiaramu: ܦܪܬ Prâth; Kar.: الفرات al-furāt; Kituruki: Fırat; Kikurdi: فرهات, Firhat) ni mto mkubwa uliopo Asia ya magharibi.
Chanzo | Uturuki ya Mashariki |
Mdomo | Ghuba ya Uajemi kwenye Shatt al Arab |
Nchi | Uturuki, Syria, Iraq |
Urefu | 2,800 km |
Kimo cha chanzo | 4,500 m |
Tawimito | Murat, Karasu |
Mkondo | 818 m³/s (wastani) |
Eneo la beseni | 765,831 km² |
Miji mikubwa kando lake | Ramadi, Falluja, Babeli |
Frati ina urefu wa takriban 2,781 km.
Baada ya kutoka katika nyanda za juu za Uturuki unaingia katika tambarare ya jangwa la Shamu na kuendelea katika Iraq unapopita kwenye maghofu ya Babeli.
Pamoja na Hidekeli (Tigri), ambao pia unatoka katika milima ya Uturuki ya Mashariki, unaunda eneo la Mesopotamia (yaani "kati ya mito"; leo kwa kiasi kikubwa inalingana na Iraq).
Karibu na mji wa Basra mito hiyo inaungana na kuitwa Shatt al Arab hadi mdomo wake katika Ghuba ya Uajemi.
Mto Frati unapita katika maeneo yasiyo na mvua, hivyo nchi zote unapopita zinajaribu kutumia maji yake kwa vituo vya kuvuta maji na malambo mbalimbali yaliyounda maziwa makubwa.
Katika Biblia umetajwa kama mto mmojawapo wa bustani walipoumbwa Adamu na Eva.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Frati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |