Mto Ruvyironza (Ruvuvu)
(Elekezwa kutoka Mto Ruvyironza)
Mto Ruvyironza una mwendo wa km 110 na ni tawimto la mto Ruvuvu ambao tena ni tawimto la Mto Kagera[1].
Kwa kuwa mto huo unaishia nchini Tanzania katika Ziwa Viktoria ambalo linatokwa na mto Naili, baadhi ya wataalamu wanahesabu urefu wa Naili kuanzia chanzo cha mto Ruvyironza nchini Burundi[2][3].
Jina linatokana na Mlima Luvironza, mkubwa kuliko yote ya Burundi, ambapo mto una chanzo chake. Mlima Luvironza una kimo cha mita 2,700 juu ya UB na uko kilomita 45 upande wa mashariki wa Ziwa Tanganyika.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "NILE". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-25. Iliwekwa mnamo 2009-10-25.
- ↑ Africa Longest River | Egypt Nile River | World Longest River | Nile White | Ancient Capital Nile
- ↑ "Encarta online encyclopedia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-13. Iliwekwa mnamo 2021-01-17.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help)
3°55′00″S 29°50′00″E / 3.9167°S 29.8333°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Ruvyironza (Ruvuvu) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |