Graviti

(Elekezwa kutoka Mvuto)

Graviti (kutoka Kiingereza: "gravity"; pia: kani ya mvutano, kanimvutano, nguvu ya uvutano, nguvu mvutano) ni kani ya uvutano iliyopo kati ya magimba yote ya ulimwengu. Kila gimba lenye masi linavuta magimba yote mengine yenye masi.

Mawazo ya wachoraji kuhusu kani ya mvutano.
Mwendo wa maji yanayotoka kwenye nozeli kuelekea juu unabadilishwa mwelekeo wake kwa umbo la parabola kutokana na nguvu ya graviti ya dunia.

Hii ndiyo sababu watu wanatembea ardhini ilhali hawawezi kuelea hewani: kwa sababu masi ya Dunia inawavuta kuelekea kitovu chake. Inavuta kila kitu chenye masi kuelekea kitovu chake. Na sisi pia watu wanaivuta Dunia, lakini kani hii ni ndogo mno kulingana na masi kubwa mno ya Dunia. Dunia yetu imeshikwa na mvuto mkali wa graviti ya Jua na hii ndiyo sababu ya Dunia kubaki karibu na Jua katika obiti na haiwezi kutoroka kwenda mbali na Jua.

Jiwe likitupwa hewani, litaanguka chini. Hii ni kwa sababu, ingawa kani ya mkono ilipeleka jiwe kwenda juu, kani ya graviti ya Dunia inapunguza kasi ya jiwe na hatimaye inalirudisha jiwe ardhini.

Tabia ya kuvutana inaonekana vyema kati ya Dunia na Mwezi. Dunia ni kubwa, inauvuta Mwezi na kuushika kwenye njia yake ya kuzunguka Dunia. Lakini wakati huohuo Mwezi unavuta pia Dunia na hii inaonekana baharini katika mabadiliko ya maji kupwa na maji kujaa kila siku. Maji ya bahari huvutwa na Mwezi kiasi kwamba kwenye sehemu ya Dunia inayotazama Mwezi, maji ya bahari yaliyo moja kwa moja chini ya Mwezi huinuliwa kiasi nusu mita juu ya wastani wa usawa wa bahari yote.

Isaac Newton anajulikana kama mtaalamu aliyeweza kueleza graviti kwa mara ya kwanza kama utaratibu wa kimsingi wa sayansi.

Atom editor logo black.svg Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Graviti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.