Kindi (mnyama)
(Elekezwa kutoka Myosciurus)
Kindi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kindi-jua kijivu (Heliosciurus gambianus)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusufamilia 5; jenasi 8 katika Afrika:
|
Kindi ni wanyama wadogo wa familia Sciuridae. Spishi nyingine huitwa kidiri au kuchakulo. Wanatokea Amerika, Ulaya, Asia na Afrika na wamewasilishwa katika Australia. Takriban spishi zote huishi mitini, lakini kuchakulo huishi ardhini. Mkia wa kindi una urefu karibu na ule wa mwili, pengine zaidi. Hula mbegu, makokwa, matunda, nyoga, matumba na machipukizi. Wakati ambapo chakula cha kimea ni adimu, kindi hula chakula cha kinyama pia, k.f. wadudu, mayai, ndege wadogo, makinda ya nyoka na wagugunaji wadogo. Spishi kadhaa za tropiki hula wadudu kushinda chakula cha kimea.
Mwainisho
hariri- Nusufamilia Ratufinae – Kindi majitu (jenasi 1, spishi 4)
- Nusufamilia Sciurillinae – Kindi kibete wa Amerika (spishi 1)
- Nusufamilia Sciurinae
- Kabila Sciurini – Kindi wa Amerika, Ulaya na Asia (jenasi 5, mnamo spishi 38)
- Kabila Pteromyini – Kindi warukaji wa Asia (jenasi 15, mnamo spishi 45)
- Nusufamilia Callosciurinae
- Kabila Callosciurini – Kindi wazuri wa Asia (13 genera, nearly 60 species)
- Kabila Funambulini – Kindi milia wa Asia (jenasi 1, spishi 5)
- Nusufamilia Xerinae – Kuchakulo, kindi wa Afrika na vidiri
- Kabila Xerini – Kuchakulo wa Afrika (jenasi 3, spishi 6)
- Kabila Protoxerini – Kindi na vidiri (jenasi 6, mnamo spishi 50)
- Kabila Marmotini – Kuchakulo wa Ulaya, Asia na Amerika (jenasi 6, mnamo spishi 90)
Spishi za Afrika
hariri- Atlantoxerus getulus, Kuchakulo wa Barbari (Barbary Ground Squirrel)
- Epixerus ebii, Kindi-mwale (Ebian's Palm Squirrel, Western Palm Squirrel au Temminck's Giant Squirrel)
- Funisciurus anerythrus, Kindi-miraba wa Thomas (Thomas's Rope Squirrel)
- Funisciurus bayonii, Kindi-miraba wa Lunda (Lunda Rope Squirrel)
- Funisciurus carruthersi, Kindi-miraba Milima (Carruthers's Mountain Squirrel)
- Funisciurus congicus, Kindi-miraba wa Kongo (Congo Rope Squirrel)
- Funisciurus isabella, Kindi-miraba wa Gray (Lady Burton's Rope Squirrel au Gray's Four-striped Squirrel)
- Funisciurus lemniscatus, Kindi-miraba Utepe (Ribboned Rope Squirrel)
- Funisciurus leucogenys, Kindi-miraba Kichwa-machungwa (Red-cheeked Rope Squirrel)
- Funisciurus pyrropus, Kindi-miraba Miguu-myekundu (Fire-footed Rope Squirrel)
- Funisciurus substriatus, Kindi-miraba wa Kintampo (Kintampo Rope Squirrel)
- Heliosciurus gambianus, Kindi-jua Kijivu (Gambian Sun Squirrel)
- Heliosciurus mutabilis, Kindi-jua Kusi (Mutable Sun Squirrel)
- Heliosciurus punctatus, Kindi-jua Mdogo (Small Sun Squirrel)
- Heliosciurus rufobrachium, Kindi-jua Miguu-myekundu (Red-legged Sun Squirrel)
- Heliosciurus ruwenzorii, Kindi-jua wa Ruwenzori (Ruwenzori Sun Squirrel)
- Heliosciurus undulatus, Kindi-jua Mashariki (Zanj Sun Squirrel)
- Myosciurus pumilio, Kindi Kibete (African Pygmy Squirrel)
- Paraxerus alexandri, Kidiri wa Alexander (Alexander's Bush Squirrel)
- Paraxerus boehmi, Kidiri wa Böhm (Böhm's Bush Squirrel)
- Paraxerus cepapi, Kidiri Kijivu (Smith's Bush Squirrel)
- Paraxerus cooperi, Kidiri-milima (Cooper's Mountain Squirrel)
- Paraxerus flavovittis, Kidiri Miraba (Striped Bush Squirrel)
- Paraxerus lucifer, Kidiri Mweusi-mwekundu (Black-and-red Bush Squirrel)
- Paraxerus ochraceus, Kidiri Ukaria (Ochre Bush Squirrel)
- Paraxerus palliatus, Kidiri Mwekundu (Red Bush Squirrel)
- Paraxerus poensis, Kidiri Kijani (Green Bush Squirrel)
- Paraxerus vexillarius, Kidiri Njano (Swynnerton's Bush Squirrel)
- Paraxerus vincenti, Kidiri wa Vincent (Vincent's Bush Squirrel)
- Protoxerus aubinnii, Kindi Mkia-mwembamba (Slender-tailed Squirrel)
- Protoxerus stangeri, Kindi Mkubwa (Forest Giant Squirrel)
- Xerus erythropus, Kuchakulo Miraba (Striped Ground Squirrel)
- Xerus inauris, Kuchakulo Kusi (Cape Ground Squirrel)
- Xerus princeps, Kuchakulo-milima (Mountain Ground Squirrel)
- Xerus rutilus, Kuchakulo Mwekundu (Unstriped Ground Squirrel)
Spishi za kabla ya historia
hariri- Hesperopetes (Mwisho wa Eocene)
- Kherem (Mwisho wa Oligocene)
- Lagrivea (Kati ya Miocene ya Ufaransa)
- Oligosciurus
- Plesiosciurus (Kati ya Miocene)
- Prospermophilus (Pliocene)
- Sciurion (Mwisho wa Miocene)
- Similisciurus (Mwisho wa Miocene)
- Sinotamias (Kati – mwisho wa Miocene)
- Vulcanisciurus (Miocene)
- Oligospermophilus (Eocene/Oligocene)
- Cedromus (Mwisho wa Oligocene)
Picha
hariri-
Kindi-mwale
-
Kindi-miraba wa Kongo
-
Kindi-jua miguu-myekundu
-
Kidiri kijivu
-
Kidiri mwekundu
-
Kidiri kijani
-
Kindi mkubwa
-
Kuchakulo wa Barbari
-
Kuchakulo miraba
-
Kuchakulo kusi
-
Kuchakulo-milima
-
Kuchakulo mwekundu
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kindi (mnyama) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |