Mkunga-ute
Mkunga-ute | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mkunga-ute wa Rasi (Eptatretus hexatrema)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nusufamilia 3 na jenasi 6:
|
Mikunga-ute ni wanyama wa baharini wa oda Myxiniformes katika ngeli Myxini wanaofanana na mikunga wa kawaida lakini ni wanyama tofauti sana. Wao ni ukoo wa kale wa samaki bila mataya. Ndio wanyama pekee wanaojulikana walio na fuvu lakini wasio na uti wa mgongo, ingawa wana vetebra zilizonywea[1]. Pamoja na mikunga wafyonzaji (ngeli Hyperoartia) wanaunda ngeli ya juu Cyclostomata (maana: wenye kinywa cha mviringo).
Tabia
haririMwili
haririKwa kawaida urefu wa mikunga-ute ni kama m 0.5. Spishi kubwa kabisa inayojulikana ni Eptatretus goliath yenye urefu hadi sm 127, huku inaonekana kama Myxine kuoi na Myxine pequenoi hufika sm 18 tu (baadhi yao wameonwa kuwa wadogo kama sm 4).
Mikunga-ute wana mwili kama mikunga na mkia kama kafi. Ngozi ni uchi na inafunika mwili kama soksi inayopwaya. Wana fuvu ya gegedu (ingawa sehemu inayozunguka ubongo inashirikisha uo wa nyuzi hasa) na miundo kama meno iliyo na keratini. Rangi hutegemea spishi, pinki hadi kijivubuluu au nyeusi na madoa meupe yanaweza kuwapo. Macho ni madoa tu, sio macho yaliyopevuka vizuri ambayo yanaweza kutatua picha. Mikunga-ute hawana mapezi ya kweli na huwa na sharubu sita au nane kuzunguka kinywa na tundu la pua moja. Badala ya mataya ya kweli kama yale ya Gnathostomata (vertebrata wenye mataya), kinywa cha mikunga-ute kina jozi mbili za miundo kwa umbo wa chanuo yenye aina za meno kwenye bamba la gegedu linalosogea mbele na nyuma. Meno haya hutumiwa kushika chakula na kukivuta kuelekea koromeo[2].
Ngozi inaunganishwa na mwili kwenye jongo la katikati la mgongo na kwenye tezi za ute na hujaa na karibu na theluthi ya kiasi cha damu ya mwili, ikitoa hisia ya gunia lililojaa na damu. Inadhaniwa kuwa hii ni utohozi kwa kukabiliana na mashambulio ya mbuai[3]. Ngozi ya mkunga-ute wa Atlantiki, mwakilishi wa nusufamilia Myxininae, na mkunga-ute wa Pasifiki, mwakilishi wa nusufamilia Eptatretinae, hutofautiana kuwa mwisho huwa na nyuzi za misuli zilizomo ndani ya ngozi. Msimamo wa kupumzika wa mkunga-ute wa Pasifiki huelekea kuwa ameviringana, huku ule wa mkunga-ute wa Atlantiki umenyooka[4].
Ute
haririMikunga-ute wanaweza kutoa viasi vikubwa vya ute au kamasi inayofanana na maziwa na kuwa na nyuzi kutoka kwenye tezi au matundu 100 kandokando ya mbavu[5]. Spishi Myxine glutinosa iliitwa kwa sababu ya ute huo. Wakishikwa kwa mkia kwa mfano hutoa ute wa nyuzi ndogondogo, ambao huongeza hadi lita 20 za dutu ya kunata ya kijelatini ukichanganywa na maji[6].
Chakula
haririWanyama wa baharini wa aina za miata karibu au juu ya sakafu ya bahari ni chanzo muhimu cha chakula, lakini mikunga-ute wanaweza kujilisha na viumbe wa bahari waliokufa au kujeruhiwa wakubwa kuliko wao wenyewe na mara nyingi hata kuingia na kutumbua miili ya viumbe hawa. Wanajulikana kwa kula nyama ya mawindo kutoka ndani[7]. Mikunga-ute wana uwezo wa kunyonya dutu ya viumbehai kupitia ngozi na matamvua, ambayo inaweza kuwa na utohozi kwa maisha ya kuokoteza, na kuwawezesha kuongeza fursa adimu za kujilisha.
Picha
hariri-
Eptatretinae (Pacific hagfish Eptatretus stoutii)
-
Mikunga-ute wa Pasifiki wakila
-
Myxinae (Atlantic hagfish Myxine glutinosa)
Marejeo
hariri- ↑ Reece, Jane (2014). Campbell Biology. Boston: Pearson. ku. 717. ISBN 0321775651.
- ↑ Hyperotreti Archived 6 Februari 2013 at the Wayback Machine.. Tree of Life
- ↑ The world's fastest shark is no match for a sack of flaccid hagfish skin
- ↑ "Comparative Biomechanics of Hagfish Skins SICB - 2017 meeting - Abstract Details". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-21. Iliwekwa mnamo 2018-09-29.
- ↑ Rothschild, Anna. "Hagfish slime: The clothing of the future?", BBC News, 2013-04-01. Retrieved on 2013-04-02.
- ↑ "Snotties at Southern Encounter". Southern Encounter Aquarium and Kiwi House. 2007-10-30. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 7, 2013. Iliwekwa mnamo 2008-10-30.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wilson, Hugh (November 2009) Hagfish – World's weirdest animals. green.ca.msn.com
Viungo vya nje
hariri- Mikunga-ute kwenye hifadhidata ya samaki Archived 3 Oktoba 2019 at the Wayback Machine.