Nabii Yehu (kwa Kiebrania יֵהוּא, Yēhû, maana yake: "YHWH ni mwenyewe"[1]; alizaliwa karne ya 10 KK) alikuwa nabii nchini Israeli katika karne ya 9 KK.

Alikuwa mwana wa Hanani, ambaye pia alikuwa nabii.

Chanzo kikuu cha historia yake ni Kitabu cha kwanza cha Wafalme, sura ya 16 na Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati, sura ya 19.

Kadiri ya kitabu cha kwanza, alimlaumu mfalme wa Israeli Baasha kwa kufuata sera ya kidini ya Yeroboamu I akamtabiria mwisho wa ukoo wake, kama ilivyotokea wakati wa mwanae Ela.

Kadiri ya kitabu cha pili, alimlaumu pia mfalme wa Yuda Yosafati kwa kufanya agano na mfalme wa Israeli Ahabu.

Tanbihi

hariri
  1. Meaning of Jehu - History and Origin Ilihifadhiwa 21 Machi 2012 kwenye Wayback Machine. – Meaning of "Jehu", Hebrew name, Meaning-of-Names.com.
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Yehu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.