Yeroboamu I
Yeroboamu I (kwa Kiebrania ירבעם השני au יָרָבְעָם; kwa Kigiriki Ιεροβοάμ; kwa Kilatini Jeroboam) alikuwa mwana wa Nebati akatawala kwa miaka 22 Ufalme wa Israeli baada ya makabila 10 ya kaskazini kuasi ukoo wa Daudi wakati wa mjukuu wake Rehoboamu.
Biblia inamhukumu hasa kwa kuanzisha sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi
Historia
haririWilliam F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu tangu mwaka 922 KK – hadi 901 KK, wakati E. R. Thiele alisema kuwa alitawala tangu 931 KK hadi 910 KK.[1]
Katika Biblia
haririAgano la Kale linamtaja mara nyingi kama chanzo cha dhambi kuu ya Waisraeli ambayo hatimaye ilisababisha ufalme uangamizwe na Waashuru katika karne ya 8 KK.
Tanbihi
hariri- ↑ Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yeroboamu I kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |