Nunzio Sulprizio (Pescosansonesco, Pescara, 13 Aprili 1817Napoli, 5 Mei 1836) alikuwa mhunzi mwanagenzi wa Italia.[1][2]

Mt. Nunzio.

Katika maisha yake mafupi kama yatima dhaifu na mwenye ugonjwa wa kudumu mguuni alisifiwa kwa maadili yake. Alistahimili mateso yote kwa utulivu na furaha, akiwahudumia na kuwafariji wagonjwa wengine, na akiwa fukara mwenyewe alijitahidi kusaidia alivyoweza maskini wote.

Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 1 Desemba 1963 baada ya miujiza miwili kutokea kwa maombezi yake.[1] Halafu alitangazwa na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 14 Oktoba 2018.

Sikukuu ya Mt. Nunzio inaadhimishwa tarehe 5 Mei, siku ya kifo chake[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 "Blessed Nuntius Sulprizio". Saints SQPN. 29 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 12 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Beato Nunzio Sulprizio". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 12 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.