Nuru Inyangete

Mtaalamu wa sanaa na sayansi ya usanifu majengo nchini Tanzania

Nuru Susan Nyerere Inyangete (alizaliwa 6 Desemba 1961) ni mtaalamu wa sanaa na sayansi ya Usanifu majengo nchini Tanzania. [1][2].

Nuru Inyangete
Amezaliwa6 Desemba 1961
UtaifaMtanzania
Kazi yakeMsanifu majengo
MwenzaProf. Charles Inyangete
WatotoEbony Neema Inyangete (1992) na Eno Melanie Inyangete (1994)

Nuru ameshika nafasi ya ukurugenzi kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo Epitome Architects Limited ambapo ni mkurugenzi mtendaji[3][4] [5]. Amejikita zaidi kwenye usanifu wa kijani na endelevu, usanifu mazingira na usanifu wa ndani.

Familia hariri

Nuru alizaliwa kwenye familia ya Lulu Kimbe na Joseph Kizurira Nyerere, mdogo wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere[6] [7]. Ni mke wa profesa Charles George Inyangete, ambaye alioana naye tarehe 6 Julai 1991 jijini London nchini Uingereza. Ni mama wa watoto wawili, Ebony Neema Inyangete (1991) na Eno Melanie Inyangete (1994).

Elimu hariri

Nuru alipata elimu ya sekondari kutoka shule ya sekondari WeruWeru iliyopo Kilimanjaro, Tanzania. Alifaulu vizuri na kuendelea na elimu ya sekondari ya juu shule ya sekondari Tambaza, Dar es Salaam, Tanzania.

Ana shahada ya uzamili kwenye sayansi ya ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, Uingereza. Pia alisoma shahada za kwanza 2, moja kwenye usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na nyingine sayansi ya usanifu (Bachelor of Science in Architectural Studies), zote akizipata kutoka Chuo hichohicho kati ya mwaka 1987 na 1989.

Kazi hariri

Nuru ana uzoefu wa miaka zaidi ya 25 katika usanifu na ujenzi. Amefanya kazi nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza, Nigeria na Tanzania. Amekua akifanya kazi kama mbunifu na mkurugenzi wa miradi mbalimbali ihusianayo na usanifu na ujenzi wa makazi, sehemu za biashara, majengo ya taasisi, usanifu wa ndani na usanifu endelevu[8][9].

Pia ametumikia kwenye bodi za taasisi mbalimbali zikiwemo bodi ya wasanifu majengo ya Tanzania (Architects and Quantity Surveyors Registration Board of Tanzania - AQRB) kama mwanzilishi na mwanachama, pamoja na mamlaka ya ununuzi ya Tanzania (Public Procurement Appeals Authority of Tanzania - PPAA)[10][11].

Kazi muhimu hariri

  • Miradi ya usanifu, ushauri wa kisanifu na ujenzi wa makazi nafuu na nyumba za jamii, miundombinu ya usafiri ya kisasa na majengo ya taasisi huko nchini Nigeria
  • Usanifu na ujenzi wa makazi ya jamii, biashara na taasisi nchini Tanzania kama vile majengo ya taasisi zikiwemo benki kuu ya Tanzania na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (National Social Security Fund) na majengo ya makazi yakiwemo makazi ya South Beach, kisota na ya shirk la nyumba Tanzania
  • Usanifu wa ofisi za shirika la kimataifa la kazi nchini Tanzania, Kenya, Somalia na Uganda
  • Zaidi ya miradi 22 ya office fit out and sehemu za burudani na starehe katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania

Tuzo hariri

  • Medali ya fedha katika ubora wa usanifu kutoka baraza la mji wa zamani wa Strathclyde (mwanamke wa kwanza kupata medali hiyo)
  • Mshindi wa kwanza wa mradi bora wa jengo la biashara kutoka bodi ya wasanifu majengo ya Tanzania mwaka 2008
  • Mshindi wa tatu wa mradi bora kwenye eneo la maendeleo ya miundombinu ya kijamii mwaka 2011
  • Mshindi wa kwanza wa mashindano ya usanifu ya shirika la kimataifa la kazi (ILO)

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nuru Inyangete kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.