Okavango (pia: Okovango; katika Angola: Kubango au Cubango) ni mto wa Afrika ya kusini-magharibi. Unaanza nchini Angola katika milima ya Bié inapojulikana kwa jina la Kubango. Mwendo wake wa km 1600 ni kusini tu hadi jangwa la Kalahari unapoishia kwenye delta ya barani. Katika kusini ya Angola ni mpaka na Namibia. Unapita nchi ya Namibia mwanzoni wa kishoroba ya Caprivi na kuendelea Botswana Unapoishia jangwani katika delta yake.

Mto wa Okavango
Feri juu ya mto Okavango nchini Botswana
Chanzo Nyanda za juu za Bié (Angola)
Mdomo Delta ya barani katika jangwa la Kalahari, Botswana
Nchi Angola, Namibia, Botswana
Urefu 1,600 km
Kimo cha chanzo 1,780 m
Mkondo 10,000,000,000 m³/mwaka (inaweza kukauka kwa muda)
Eneo la beseni 721.258 km²
Delta ya Ovango inavyoonekana kutoka angani

Jina la mto limepatikana kutoka kabila la Wakavango.

Chanzo cha mto ni kusini KWa mji wa Vila Nova (Angola) katika milima ya Bié kwenye kimo cha mita 1,780. Mwanzoni mwendo wake ni wa haraka kuna maporomoko madogo. Halafu mto ni mpaka kati ya Angola na Namibia. Baada ya kupokea tawimto la Kwito unaingia Namibia unapopita kanda nyembamba ya kishoroba ya Caprivi kwa kilomita chache. Kabla ya kuvuka mpaka wa Botswana mto unashuka mita 4 kwenye maporomoko ya Popa.

Takriban km 70 ndani ya Botswana mwendo wa mto unapanuka na kugawanyika kuwa delta ya barani yenye zaidi ya km² 16,000.

Delta hiyo imeorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Okavango kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.