Olena Pchilka
Olha Petrivna Kosach (anajulikana zaidi kwa jina la Olena Pchilka; 29 Juni 1849 – 4 Oktoba 1930) alikuwa mchapishaji, mwandishi, mtaalamu wa ethnografia, mkalimani, na mwanaharakati wa haki za kiraia wa nchini Ukraine. Alikuwa dada wa Mykhailo Drahomanov na mama wa Lesya Ukrainka, Olga Kosach-Kryvyniuk, Mykhajlo Kosach, Oxana Kosach-Shymanovska, Mykola Kosach, Izydora Kosach-Borysova na Yurij Kosach . [1]
Miaka ya mwanzo
haririPchilka alizaliwa huko Hadiach, katika familia ya mmiliki wa ardhi Petro Yakymovych Drahomanov. Alipata elimu ya msingi nyumbani na akamaliza elimu yake katika shule ya bweni ya Noble Maidens ( Kyiv ) mnamo mwaka 1866. Aliolewa na Petro Antonovych Kosach mnamo mwaka 1868 na hivi karibuni alihamia Novohrad-Volynsky, ambapo alifanya kazi. Binti zake kama Lesya Ukrainka alizaliwa huko. Pchilka labda ndiye, mshairi wa kike anayejulikana zaidi wa nchini Ukraini. Alifariki huko Kyiv, akiwa na umri wa miaka 81. [2]
Pchilka alirekodi nyimbo za kitamaduni, mila na desturi za watu, na akakusanya mapambo ya kitamaduni ya watu huko Volhynia ,na baadaye kuchapisha utafiti wake.
Alichapisha kazi nyingi, na alikuwa mchapa kazi katika harakati za kupigania haki za wanawake , haswa kwa ushirikiano na Natalia Kobrynska ambaye naye alichapisha almanaka huko Lemberg "Pershyi nok".
Mnamo 1913, Lesya Ukrainka alikufa, Olena Pchilka alihama kutoka Kyiv kwenda Gadyach, na ataishi katika nyumba ambayo alitumia utoto wake.[3]
Ukalimani
haririPchilka pia alikuwa mkalimani na alitafsiri kazi nyingi maarufu katika lugha ya Kiukreni, kama vile Nikolai Gogol, Adam Mickiewicz, Aleksandr Pushkin na zinginezo.
Kazi
haririMiongoni mwa kazi zake maarufu zaidi ni:
- "Tovaryshky" (Comradesses, 1887),
- "Svitlo dobra i lyubovi"(The light of goodness and love, 1888)
- "Soloviovyi spiv" (Nightingale singing, 1889),
- "Za pravdoyu" (For a truth, 1889),,
- "Artyshok" ( Artichoke, 1907),
- "Pivtora oseledsya" (One and a half herring, 1908)
- a play "Suzhena ne ohuzhena" (1881),
- a play "Svitova rich" (World thing, 1908) and others
Marejeo
hariri- ↑ Olga, Kosach-Kryvyniuk (1970). Леся Українка: Хронологія життя і творчості. New-York.
{{cite book}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) - ↑ Aleksandr Mikhaĭlovich Prokhorov (1982). Great Soviet encyclopedia. Macmillan. uk. 185.
- ↑ "Життя гадяцької інтелігенції: якою була Садиба Драгоманових та куди поділась нині - ipoltavets.com" (kwa Kiukraini). 2022-11-04. Iliwekwa mnamo 2022-11-08.