Onufri mkaapweke

Onufri mkaapweke (pia "Nofer"; kwa Kigiriki Ὀνούφριος, labda kutoka Kimisri "Unnufer", yaani "Mwenye furaha daima"[1]) aliishi miaka sitini au sabini jangwani katika Misri Kusini katika karne ya 4 au ya 5 bila kuonekana na mtu, kiasi kwamba hakuvaa nguo yoyote.

Picha takatifu ya Mt. Onufri.

Habari zake zimesimuliwa na Pafnusi wa Tebe, ambaye peke yake alifaulu kumuona mwishoni mwa maisha yake na kumzika.[2]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Juni[3][4].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Gardiner, Alan H. (1936). "The Egyptian Origin of Some English Personal Names". Journal of the American Oriental Society (American Oriental Society) 56 (2): 189–97. doi:10.2307/594666 . ISSN 0003-0279 .
  2. Peter W. Parshall; Rainer Schoch, National Gallery of Art (U.S.); Origins of European Printmaking (Yale University Press, 2005), 318.
  3. Martyrologium Romanum
  4. https://catholicsaints.info/saint-onuphrius/

VyanzoEdit

  • Alban Butler, Paul Burns; Butler’s Lives of the Saints (Continuum International Publishing Group, 2000)

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.