Manikwe
Manikwe wa kawaida (Malapterurus electricus)
Manikwe wa kawaida (Malapterurus electricus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Siluriformes (Samaki kama kambale)
Familia: Malapteruridae
Jordan, 1923
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 21:

Manikwe au nyika ni samaki wa maji baridi wa familia Malapteruridae katika oda Siluriformes ambao wanatokea Afrika tu. Familia hii ina jenasi 2 na spishi 21. Spishi kadhaa za familia hii zina uwezo wa kutoa mrusho wa umeme hadi volti 350 wakitumia mabamba ya umeme ya ogani maalumu. Manikwe hupatikana katika Afrika ya kitropiki na Mto Naili. Hukiakia usiku na hula nyama. Spishi fulani hujilisha hasa samaki wengine wakiwaondelea mawindo yao nguvu kwa mirusho ya umeme, lakini wengine hula kitu chochote kwa sakafu ya maji k.m. invertebrata, mayai ya samaki na takataka.

Maelezo

hariri

Malapteruridae ni kundi pekee la samaki kama kambale walio na ogani zinazotoa umeme na zilizokua vizuri; hata hivyo, mifumo ya udakaji wa umeme imeenea katika samaki kama kambale. Ogani ya umeme hutoka kwa misuli ya mbele ya mwili na hufunika ukuta wa uwazi wa mwili. Manikwe hawana pezimgongo wala miiba kwenye mapezi. Wana jozi tatu za sharubu (jozi ya pua haipo). Kibofuboya kina vyumba vya nyuma vilivyorefuka, vyumba viwili katika jenasi Malapterurus na tatu katika Paradoxoglanis.

Manikwe mkubwa kabisa anaweza kufika urefu wa m 1.2 bila mkia na uzito wa kg 20, lakini takriban spishi zote nyingine huzifika zaidi ya sm 30 tu.

Manikwe na watu

hariri

Manikwe wa Naili walijulikana sana kwa Wamisri wa kale. Wamisri walitumia mrusho wao wa umeme wakati wa kutibu maumivu ya yabisi. Waliweza kutumia samaki wadogo tu, kwa sababu samaki wakubwa wanaweza kutoa mrusho wa umeme wa volti 300 hadi 400. Wamisri wameonyesha samaki hawa katika michoro yao ya ukuta na mahali pengine; taswira ya kwanza ya manikwe inayojulikana ni kwenye kipande cha grife cha mtawala wa Misri kabla ya utawala wa kinasaba, aliyeitwa Narmer, mnamo 3100 KK. Waliitwa "samaki wenye hasira" kwa Kimisri.

Mrusho wa manikwe hutumiwa kwa kuwaondolea mawindo nguvu na kwa ulinzi. Haujulikani kuleta mauti kwa wanadamu, lakini manikwe wakubwa wanaweza kumwondolea mtu mzima nguvu. Manikwe wadogo wanatoa mkondo mdogo sana na huu unahisi tu kama mnyeo kwa wanadamu.

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri

Spishi za sehemu nyingine za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri