Perpetui wa Tours
Perpetui wa Tours (alifariki Tours, leo nchini Ufaransa, 30 Desemba 490 BK) alikuwa askofu wa 6 wa mji huo kwa miaka 30 baada ya ndugu yake Eustoki wa Tours na kabla ya ndugu yake mwingine, Volusiano wa Tours.
Alijenga basilika la Mt. Martino na makanisa mengine mengi kwa heshima ya watakatifu pamoja na kurudisha jimboni mwake desturi ya kufunga chakula na kukesha [1].
Gregori wa Tours aliandika juu yake[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Desemba[3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ [1]
- ↑ Gregory, History of the Franks.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
hariri- (Kiingereza) Saint Patrick's Saint Index: April 8 - St.Perpetuus Ilihifadhiwa 8 Aprili 2019 kwenye Wayback Machine.
- (Kiingereza) Catholic Encyclopedia: St. Perpetuus
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |