Peter Chanel

Petro Shanel (12 Julai 180328 Aprili 1841) alikuwa padri mmisionari wa Kanisa Katoliki.

Mt. Peter Chanel.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Aprili[1].

MaishaEdit

Petro Shanel alizaliwa mjini Cuet, Ufaransa mwaka 1803.

Baada ya kupata upadrisho alishughulika na uchungaji nchini mwake kwa miaka michache.

Halafu aliingia Shirika la Maria, akaenda Oceania kuhubiri Injili.

Licha ya matatizo mengi alifaulu kuwaongoa watu kadhaa. Kwa sababu ya kuchukiwa kwa imani ya Ukristo, alikamatwa na kuuawa kwa kupigwa rungu katika kisiwa cha Futuna, mwaka 1841.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

MarejeoEdit

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1341
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.