Petro, Valabonso na wenzao
Petro, Valabonso na wenzao Sabiniano, Vistremundo, Abensi na Yeremia (walifariki Cordoba, Hispania, 7 Juni 851) walikuwa wamonaki wa Cordoba waliouawa kwa kukatwa kichwa na Waislamu waliotawala nchi hiyo kwa sababu waliungama hadharani imani yao ya Kikristo [1].
Petro alikuwa padri na Valabonso shemasi kijana.
Dhuluma ilipoanza, walijitokeza kwa hiari yao mahakamani kujadiliana kuhusu ukweli wa dini.
Taarifa zao ziliandikwa na Eulogi wa Kordoba[2] [3].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/56220
- ↑ Latin writings of Eulogius pdf downloads at documentacatholicaomnia.eu
- ↑ Complete Works of Eulogius of Cordoba English translations of Eulogius' writings.
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo
hariri- Tolan, John, Medieval Christian Perceptions of Islam, New York: Routledge, 2000. ISBN|0-8153-1426-4
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |