Peter Chanel

(Elekezwa kutoka Petro Chanel)

Petro Shanel (12 Julai 180328 Aprili 1841) alikuwa padri mmisionari wa Kanisa Katoliki.

Mt. Peter Chanel.

Ametambuliwa rasmi na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 17 Novemba 1889, halafu na Papa Pius XII kuwa mtakatifu kama mfiadini tarehe 12 Juni 1954.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Aprili[1].

Maisha

hariri

Petro Shanel alizaliwa mjini Cuet, Ufaransa mwaka 1803.

Baada ya kupata upadrisho alishughulika na uchungaji nchini mwake kwa miaka michache, akiwajibika hasa kwa ajili ya wakulima na malezi ya vijana.

Halafu aliingia Shirika la Maria, akatumwa akatumwa katika visiwa vya Oceania pamoja na wenzake kadhaa kuhubiri Injili mahali ambapo ilikuwa haijatangazwa.

Licha ya matatizo mengi alifaulu kwa upole wake kuwaongoa watu kadhaa katika kisiwa cha Futuna, akiwemo mwana wa mfalme. Kwa sababu ya kuchukiwa kwa imani ya Ukristo, huyo kwa hasira aliagiza akamatwe na kuuawa kwa kupigwa rungu mwaka 1841.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Marejeo

hariri
  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1341
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.