Petro wa Argo (pia: Petro mtendamiujiza; kwa Kigiriki: Άγιος Πέτρος ο Θαυματουργός[1] ; Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, karne ya 9 - Argos, Ugiriki, 922 hivi) alikuwa mzaliwa wa familia tajiri yenye maadili bora, halafu mmonaki na hatimaye askofu wa Argos na Nauplion.

Mt. Petro alivyochorwa.

Kwa upendo mkubwa alijitahidi kusaidia fukara na kukomboa watumwa, mbali ya kujenga umoja kati ya Wakristo [2]

Maandishi yake yanapatikana katika mkusanyo wa Patrologia Graeca[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Mei[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. St Peter the Wonderworker and Bishop of Argos. OCA – Lives of the Saints.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/51730
  3. Great Synaxaristes (Kigiriki): Ὁ Ἅγιος Πέτρος Ἐπίσκοπος Ἄργους. 3 Μαΐου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.
  4. Ott, M. (1911). Oil of Saints. In The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. Retrieved June 6, 2015 from New Advent: http://www.newadvent.org/cathen/11228d.htm, after Acta Sanctorum, May, I, 432
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.