Petro wa Betancur

Petro wa Betancur (Tenerife, Hispania, 21 Machi 1626 - Antigua, Guatemala 25 Aprili 1667), alikuwa mmisionari kutoka Hispania katika Amerika ya Kati.

Sanamu ya Petro wa Mt. Yosefu Betancur katika Pango la Mt. Hermano Pedro (Tenerife).

Alijulikana kama "Mt. Fransisko wa Amerika", naye ni mtakatifu wa kwanza mzaliwa wa visiwa vya Kanaria, pia anahesabiwa wa kwanza katika Guatemala na Amerika ya Kati.

Petro alitambulikana kwa unyenyekevu na ugumu wa maisha katika kutekeleza huruma kwa wengine.[1]

Mwanashirika wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko, alianzisha pia shirika la kwanza la barani Amerika, "Ndugu wa Kiume na wa Kike wa Bethlehemu". Baada ya kufutwa, lilifufuliwa tarehe 16 Januari 1984.

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 22 Juni 1980, halafu mtakatifu tarehe 30 Julai 2002. [1]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Aprili[2].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.