Petro wa Moutiers

Petro wa Moutiers, O.Cist. (Saint-Maurice-de-l'Exil, 1102 - Bellevaux, 14 Septemba 1174) alikuwa askofu wa mji huo, leo nchini Ufaransa[1].

Baada ya kukariri Zaburi zote, akiwa na umri wa miaka 20 alijiunga na monasteri ya Wasitoo. Hata wazazi wake na ndugu zake watatu wakawa wamonaki[2].

Miaka 10 baadaye alifanywa abati wa monasteri mpya[3], na miaka 10 tena baadaye askofu kwa pendekezo la Bernardo wa Clairvaux.

Aliongoza vizuri ajabu jimbo lake akilitembelea lote, akisaidia maskini[4] na kumpinga kaisari Frederick I Barbarossa aliyemsimamisha antipapa Vikta IV dhidi ya Papa Aleksanda III. Pia aliteuliwa kupatanisha wafalme.

Papa Selestini III alimtangaza mtakatifu mwaka 1191.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[5].

Tazama pia Edit

Tanbihi Edit

Marejeo Edit

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. London:Penguin Books, 3rd edition, 1995. ISBN|0-14-051312-4.
  • Rabenstein, Katherine (August 1999). Peter of Tarentaise, OSB Cist. B.. Saints O' the Day for May 8. Jalada kutoka ya awali juu ya 6 February 2007. Iliwekwa mnamo 2012-02-23.

Viungo vya nje Edit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.