Msonobari

(Elekezwa kutoka Pinaceae)
Msonobari
Msonobari mweusi (Pinus nigra)
Msonobari mweusi (Pinus nigra)
Koni ya kike iliyojifungua
Koni ya kike iliyojifungua
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Gymnospermae (Mimea isiyotoa maua)
Divisheni: Pinophyta (Mimea iliyo na matunda kwa umbo wa koni)
Ngeli: Pinopsida (Mimea kama msonobari)
Oda: Pinales (Mimea kama msonobari)
Familia: Pinaceae (Mimea iliyo na mnasaba na msonobari)
Spreng. ex F.Rudolphi
Ngazi za chini

Jenasi 11:

Msonobari (pia msunobari au msindano) ndilo jina la kawaida la miti na vichaka ya familia Pinaceae, lakini majina mengine hutumika pia kwa spishi za jenasi fulani, k.m. mberoshi (Abies), msedra (Cedrus), mteashuri (Larix) na msprusi (Picea). Miti hii huitwa mikoni pia, pamoja na spishi nyingine za oda Pinales, kwa sababu matunda yao yana umbo la koni. Kwa lugha nyingine huitwa “miti-sindano”, kwa sababu majani ya spishi nyingi yana umbo la sindano.

Maelezo hariri

Misonobari ni miti (vichaka kwa nadra) inayokua kutoka urefu wa mita 2 hadi 100. Inabeba majani mwaka mzima (ila spishi za Larix na Pseudolarix zinazopoteza majani wakati wa baridi) na kutoa resini. Inabeba maua ya kike na ya kiume kwa mti mmoja na matawi yaliyopo mkabala au katika vetisili na majani yafananayo na sindano ambayo yamewekwa katika umbo la kujiviringa. Viinitete vya misonobari vina kotiledoni tatu hadi 24.

Koni za kike ni kubwa na zina ubao kwa kawaida, kwa urefu wa sm 2-60, na zina magamba mengi kwa umbo la kujiviringa na mbegu mbili zenye bawa kwa kila gamba. Koni za kiume ni ndogo, kwa urefu wa sm 0.5-6.0, na zinaanguka haraka baada ya uchavushaji. Kueneza kwa chavua ni kwa upepo. Mtawanyiko wa mbegu ni kwa upepo hasa, lakini spishi fulani zina mbegu kubwa zilizo na mabawa yaliyopunguzika na zinaenezwa na ndege. Hitilafu katika ukubwa wa koni katika familia hii inaelekea kutokana na hitilafu ya mifumo ya kueneza mbegu iliyopo katika mazingira yao kwa muda. Misonobari yote yenye mbegu kwa uzito wa chini ya mg 90 inaonekana kutoholewa kwa mtawanyiko kwa upepo. Ile yenye mbegu kubwa zaidi ya mg 100 zinaelekea zaidi kunufaika kutokana na mageuzi ambayo yanasaidia mtawanyiko kwa wanyama, kwa ndege hasa. Misonobari inayoendelea katika maeneo ambapo kindi ni tele haionekani kuwa na mabadiliko kwa ajili ya mtawanyiko kwa ndege.

Taratibu za kinga hariri

Kinga za misonobari huenea katika gome la miti. Sehemu hii ya mti huchangia mpaka wa kujihami dhidi ya maadui wa nje. Kuna aina za kinga zilizopo katika gome sikuzote na aina nyingine zinazochochewa.

Kinga zilizopo hariri

Kwa kawaida kinga hizi ni mstari wa kwanza wa kinga uliotumiwa dhidi ya maadui na zinaweza kushirikisha seli zilizo na ukuta ngumu, seli za peridermi zenye lignini na kemikali za upili kama vile fenoli na resini. Kinga hizi zipo daima na kupatia kinga ya haraka dhidi ya mashambulizi lakini pia zinaweza kushindwa na maadui ambao wamegeuza mabadiliko dhidi ya taratibu hizi za kinga. Baadhi ya kemikali za upili za kawaida zinazotumiwa na misonobari ni fenoli au polifenoli. Kemikali hizi za upili huhifadhiwa kwenye vakuoli za seli za parenkima zenye polifenoli katika floemu ya upili.

Kinga zinazochochewa hariri

Maitikio ya kinga zinazochochea yanahitajika kuanzishwa na ishara fulani kama vile uharibifu kwa walamajani au ishara nyingine kutoka viumbehai. Utaratibu wa kawaida wa kinga yanayochochea ambao hutumiwa na misonobari ni resini. Resini pia ni moja ya kinga za msingi zinazotumika dhidi ya mashambulizi. Resini ni kinga za muda mfupi ambazo hujumuisha mchanganyiko tata wa mono- (C10) na seskwitapeni (C15) vukifu na asidi za resini ya ditapeni zisizovukiza (C20). Huzalishwa na kuhifadhiwa katika mahali maalum pa unyaji panapojulikana kama mifereji, malengelenge au mawazi ya resini. Resini zina uwezo wa kuondoa, kutega na kujikinga dhidi ya wapinzani, na pia zinahusishwa katika kuziba jeraha. Ni utaratibu wa ufanisi wa kinga kwa sababu zina athari za sumu na kuzuia kwa wavamizi, kama vile wadudu au vidusia. Resini zingaliendelea kama kinga ya mabadiliko dhidi ya mashambulio ya mbawakawa wa gome. Resini moja katika misonobari iliyotafitiwa vizuri ni oleoresini. Hii imevumbuliwa kuwa baadhi muhimu ya utaratibu wa kinga wa mikoni dhidi ya mashambulio ya viumbehai. Hupatikana katika tishu za unyaji katika mashina, mizizi na majani ya miti.

Misonobari na watu hariri

Spishi nyingi za misonobari, hasa zile kubwa, hutumika kutoa mbao. Spishi fulani zinazaa mbegu zinazolika, ambazo ni maarufu katika maeneo fulani, kama nchi za Mediterranea na Amerika ya Kati. Resini za misonobare huvunwa ili kutoa terafini, nao resini ya msonobari wa Alepo hutumika kwa kukoleza retsina, aina ya divai ya Kigiriki. Hatimaye, spishi fulani, misprusi hasa, hutumika kama miti ya Krismasi. Mwanzoni msprusi wa Norwei ulipendelewa kwa kusudi hili, lakini sikuhizi spishi nyingi kiasi zinatumiwa.

Spishi za kienyeji za Afrika hariri

Spishi zilizopandwa katika Afrika hariri

Picha hariri