Ponsyo wa Cimiez (alifariki Nice, leo nchini Ufaransa, 257 hivi) alikuwa Mkristo aliyeuawa kwa ajili ya imani yake wakati wa dhuluma ya kaisari Valeriani wa Dola la Roma[1].

"Kifodini cha Mt. Ponsyo": mchoro wa Joseph Castel (1798-1853).

Inasemekana alitokea Roma alipoongokea Ukristo [2] na kuinjilisha bonde la mto Ubaye[3].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Mei[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Nominis: Saint Ponce (Kifaransa)
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/53110
  3. Vallis Montium : Histoire de la vallée de Barcelonnette p.19, Julien Coste, 1932, reissued Sabenca 1995, ISBN 2-908103-18-4
  4. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.