Powercomputers Telecommunications

Powercomputers Telecommunications Limited ni kampuni ya teknolojia na msambazaji wa Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD) iliyoidinishwa na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (Tanzania Revenue Authority)[1] nchini Tanzania.

Powercomputers Telecommunications Limited
AinaTeknolojia
Ilipoanzishwa2001
WaanzishiShakil Dharamsi
Makao MakuuDar Es Salaam, Tanzania
Idadi ya vituo11
HudumaMachine za elektroniki vya fedha(EFD),Vifaa vya Kompyuta, Programu ya Biashara, Mafunzo ya Kompyuta, Ufundi wa Teknolojia

Kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2001[2], makao makuu ni katika jiji la Dar es Salaam, pamoja na matawi 11 katika mikoa za Arusha, Dodoma, Mwanza, Moshi, Manyara, Bukoba, Iringa, Morogoro, Lindi, Mtwara, Tanga.

Mashine ya risiti ya elektroniki iliyouzwa na Powercomputers.

Historia hariri

Kampuni ya Powercomputers ni kampuni mojawapo ya kwanza katika sekta ya teknolojia katika nchi ya Tanzania.[2] Pamoja na kuuza bidhaa za komputa na programu za kibiashara, kampuni hii ina kituo cha mafunzo iliyosajiliwa na NACTE (National Council For Technical Education)[3] [4]

Zaidi na huduma hizo, kampuni hiyo inaajiri Watanzania zaidi ya 80, katika kazi za wataalamu. Waziri ya Ujenzi na Uchukuzi, Isack Kamwelwe alipongeza kampuni za Kitanzania zilizokuwa na wataalmu, kuliko kampuni za kigeni. [5]

Usambazaji za Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD) hariri

Mamlaka ya Mapato Tanzania ilichagua kampuni kumi kusambaza mashine za risiti elektroniki vya fedha (EFD), mojawapo ikiwa kampuni ya Powercomputers Telecommunications Limited. Mashine za Risiti za Kielektroniki zinasaidia mamlaka za serikali kukusanya kodi, pamoja na kuongeza takwimu za biashara nchini.

Mashine hizo zinapatikana kwa kutumia wazalishaji wafuatao:

  • Incotex 118
  • Incotex 300SM
  • HCP BEST
  • HCP Prima

Pamoja na kuuza mashine hizo, kampuni hiyo inawaelimisha Watanzania wote jinsi za kutumia mashine hizo kwa njia za video katika mtandao wa Youtube.[6][7]

Marejeo hariri

  1. "Mamlaka ya Mapato Tanzania - Wasambazaji wa Mashine za Risiti za Kielektroniki". www.tra.go.tz. Iliwekwa mnamo 2021-05-16. 
  2. 2.0 2.1 The Guardian Tanzania - Powercomputers: Leading in Total IT Solutions
  3. "Registered and Accredited Institutions – The National Council for Technical Education (NACTE)" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2021-05-16. 
  4. "New Tanzanian Centre Set For a Bright Future". NCC Education (kwa en-GB). 2011-06-06. Iliwekwa mnamo 2021-05-16. 
  5. "Engineer Kamwelwe’s says local engineers to undertake Dar Port’s eSWS". www.ippmedia.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-05-16. 
  6. EFD Incotex 181 Jinsi ya kuuza kwa mteja bila TIN Powercomputers (kwa sw-TZ), iliwekwa mnamo 2021-05-16 
  7. EFD Tremol S Namna ya kutoa X Report Powercomputers (kwa sw-TZ), iliwekwa mnamo 2021-05-16