Meridiani ya sifuri
Meridiani ya sifuri (kwa Kiingereza: Prime Meridian, Null meridian, Zero meridian) ni mstari wa meridiani unaokubaliwa kuwa mstari wa rejeo kwa kutaja longitudo za mahali duniani. Tangu mwaka 1884 meridiani hiyo ni mstari unaopita kutoka ncha ya Kaskazini hadi ncha ya Kusini kupitia paoneaanga pa Greenwich mjini London, Uingereza. Mstari wa Greenwich ni sifuri, na mistari zenye umbali wa nyuzi moja hutajwa kuwa nyuzi za longitudo upande wa mashariki au magharibi za sifuri, yaani Greenwich.
Historia ya uteuzi wa Greenwich
haririHadi mwaka ule kulikuwa na meridiani za kurejelea tofauti kati ya nchi na nchi pamoja na meridiani ya Greenwich kuwa rejeleo kwa ramani za Kiingereza. Maana Greenwich, ambayo ni pambizo la London, ilikuwa mahali pa paoneaanga pakuu pa Uingereza. Mnamo mwaka 1880 Uingereza ilikuwa nchi yenye meli nyingi duniani na idadi kubwa ya meli ilitumia ramani zilizorejelea Greenwich kwa kutaja majiranukta ya mahali.
Mwaka 1884 rais wa Marekani alikaribisha mkutano wa kimataifa "International Meridian Conference" uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 25. Mkutano ulipendekeza kutumia meridiani ya Greenwich kama "meridiani ya sifuri".
Hata hivyo, Ufaransa haukukubali mwanzoni na kwa miaka kadhaa iliyofuata ramani za Kifaransa zilionyesha meridiani ya Paris kuwa "meridiani ya sifuri".
Mfumo wa kutaja majiranukta au anwani ya kijiografia
haririMeridiani ya Greenwich huhesabiwa kuwa "0", halafu kuna nyuzi 180 upande wa mashariki na nyuzi 180 upande wa magharibi. Nyuzi ya 180 ni ya pamoja kinyume cha mstari wa Greenwich.
Nyuzi za longitudo hutajwa ama kwa kuongeza "za mashariki / East" na "za magharibi / West", au kwa kutumia namba chanya kwa nyuzi za mashariki na namba hasi kwa zile za magharibi.
Kila meridiani hukatwa na mstari wa ikweta. Sambamba na ikweta iko mistari ya duara ya latitudo inayotajwa kwa nyuzi 1-90 za kaskazini au nyuzi 1-90 za kusini.
Nchi zinazopitwa na meridiani ya sifuri
haririMstari wa longitudo Greenwich unapita kwenye nchi zifuatazo:
- Ufalme wa Muungano,
- Ufaransa,
- Hispania,
- [[Algeria,
- Mali,
- Burkina Faso,
- Togo,
- Ghana, na
- Antaktiki.
Inapita pia kwenye sehemu za
Tanbihi
hariri
Viungo vya Nje
hariri- "Where the Earth's surface begins—and ends", Popular Mechanics, December 1930