Proklo wa Konstantinopoli

Proklo wa Konstantinopoli (alifariki karibu na Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 24 Julai 446) alikuwa askofu mkuu wa mji huo kuanzia mwaka 434 hadi kifo chake[1].

Mchoro mdogo juu yake.

Alitetea kwa ushujaa imani ya kuwa Bikira Maria anastahili kuitwa Mama wa Mungu dhidi ya Nestori, mtangulizi wake kama askofu mkuu wa jimbo [2]

Ili kurudisha umoja kati ya waumini alihamishia mjini kwa maandamano ya fahari masalia ya Yohane Krisostomo. Kwa ajili hiyo Mtaguso wa Kalsedonia ulimuita "Mkuu" [3].

Anaheshimiwa tangu kale na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Oktoba[4] au 20 Novemba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/74960
  2. The works of Proclus consist of 20 sermons (some of doubtful authenticity). Daniel 1911 cites Migne, Patrologia Graeca lxv. 651) Five were published by Cardinal Mai, Daniel 1911 cites Spicilegium Romanum, iv. xliii. lxxviii. of which 3 are preserved only in a Syriac version, the Greek being lost; 7 letters, along with several addressed to him by other persons; and a few fragments of other letters and sermons. Daniel 1911 cites Socrates, Ecclesiastical History, vii. xxvi., and passim; Theophanes, sub annus 430; Tillemont, Mém. eccl. xiv. 704; AA. SS. Act. x. 639. Proclus was cited by Cardinal John Henry Newman for his work on mariology and his strong support of the conciliar dogma on the Theotokos. Proclus was cited by Cotton Mather in his work entitled Psalterium Americanum (a commentary on the Book of Psalms) for his view on the book of Psalms. Mather directly quotes Proclus in a five-line quotation about the purposes for reading the Psalms.
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/74960
  4. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Meyendorff, John (1989). Imperial unity and Christian divisions: The Church 450-680 A.D. The Church in history. Juz. la 2. Crestwood, NY: St. Vladimir's Seminary Press. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  •   Bacchus, Francis Joseph (1911). "St. Proclus". Catholic Encyclopedia. 12. New York: Robert Appleton Company.
  • Prologue from Ochrid by St. Nikolai Velimirović
  • Constas, Nicholas (2003). Proclus of Constantinople and the Cult of the Virgin in Late Antiquity: Homilies 1-5, Texts and Translations. Leiden: Brill.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.