Publia wa Antiokia

Publia wa Antiokia alikuwa mwanamke Mkristo wa karne ya 4 wa huko Antiokia, leo nchini Uturuki, ambaye, baada ya kuishi katika ndoa na kuzaa mtoto mmoja, alipofiwa mumewe alijiunga na monasteri akawa abesi wake.

Ni maarufu kwa kuongoza masista wenzake kumpinga kaisari Juliani Mwasi hadi akapigwa na kudhalilishwa naye vibaya. Kaisari huyo alipopita karibu nao, waliimba maneno ya Zaburi: «Miungu ya mataifa ni fedha na dhahabu tu», tena: «Awe sawa nayo mtu anayeitengeneza» [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Oktoba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.