Visiwa vya Malkia Elizabeth

(Elekezwa kutoka Queen Elizabeth Islands)

Visiwa vya Malkia Elizabeth (kwa Kiingereza: Queen Elizabeth Islands, Kifaransa: Îles de la Reine-Élisabeth) ndio kundi la visiwa kaskazini mwa Funguvisiwa la Aktiki ya Kanada. Kiutawala visiwa hivi vimegawanyika baina ya Nunavut na Northwest Territories za Kanada. Visiwa vya Malkia Elizabeth vimefunikwa kabisa kwa barafu ilhali vina takriban asilimia 14 za eneo la barafu na theluji duniani [1] ukiondoa ngao za barafu za Greenland na Antaktiki.

Visiwa vya Malkia Elizabeth, kaskazini mwa Kanada.



</br>     Nunavut

Visiwa hivyo vilipewa jina kwenye mwaka wa 1953, baada ya kutawazwa kwake Elizabeth II kuwa malkia wa Kanada. Kabla ya hapo vilijulikana kama Parry Archipelago kwa zaidi ya miaka 130 tangu kupitiwa na mpelelezi Mwingereza Sir William Parry mnamo 1820.

Jiografia

hariri

Kulingana na atlasi ya Kanada kuna visiwa vikubwa 34 na vidogo 2,092 katika funguvisiwa hilo[2]. Kisiwa kikubwa ni Ellesmere Island iliyo na km² 196,235.

Visiwa kwa pamoja vina eneo la kilomita za mraba 419,061[2].

Visiwa hufunika eneo linalofanana na umbo la pembetatu ilhali inapakana na Mlangobahari wa Nares upande wa mashariki, mlangobahari wa Parry upande wa kusini na Bahari ya Aktiki upande wa kaskazini na magharibi.

Visiwa vilivyo vingi havina watu isipokuwa kuna vituo vya utafiti wa tabianchi.

Marejeo

hariri
  1. Sharp, Martin; Burgess, David O.; Cogley, J. Graham; Ecclestone, Miles; Labine, Claude; Wolken, Gabriel J. (9 Juni 2011). "Extreme melt on Canada's Arctic ice caps in the 21st century" (PDF). Geophysical Research Letters. 38 (11): n/a. Bibcode:2011GeoRL..3811501S. doi:10.1029/2011GL047381. Iliwekwa mnamo 20 Februari 2014.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Sea islands". Atlas of Canada. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 22, 2013. Iliwekwa mnamo Januari 22, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Malkia Elizabeth kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.