Rachel Carson

Mwanabiolojia wa baharini na mhifadhi kutoka Marekani

Rachel Louise Carson (27 Mei 1907 - 14 Aprili 1964) alikuwa mwanasayansi wa kibiolojia kutoka nchini Marekani.

Rachel Carson mwaka 1940

Carson alianza kazi yake kama mwanabiolojia wa maji katika Ofisi ya Uvuvi ya Umoja wa Mataifa.

Maisha na kazi hariri

Rachel Carson alizaliwa 27 Mei 1907, kwenye shamba la familia karibu na Springdale, Pennsylvania, juu kidogo ya Mto Allegheny kutoka Pittsburgh.

Carson alianza kuandika hadithi (mara nyingi huhusisha wanyama katika hadithi zake) akiwa na umri wa miaka nane na alikuwa na hadithi yake ya kwanza iliyochapishwa akiwa katika umri wa miaka kumi.

Alifurahia sana St. Nicholas Magazine (ambayo ilisambaza hadithi za kwanza), kazi za Beatrix Potter, na riwaya za Gene Stratton-Porter, na katika miaka yake ya ujana, Herman Melville, Joseph Conrad na Robert Louis Stevenson.

Carson alisoma shule ya msingi ya Springdale kupitia daraja la kumi, kisha alikamilisha shule ya sekondari karibu na Parnassus, Pennsylvania, alihitimu mwaka 1925 na darasa lake lilikuwa na wanafunzi 45.

Katika Chuo cha Wanawake cha Pennsylvania (leo kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Chatham). Carson alianza kusoma Kiingereza, lakini alibadilisha na kuchukua biolojia mwezi Januari 1928. Alisomea elimu ya ufundi wa Kibiolojia katika maabara.

Aliendelea na masomo yake ya zuolojia (biolojia ya wanyama) katika Chuo kikuu cha Johns Hopkins mwishoni mwa mwaka 1929.

Msimamizi wa Carson, alifurahia mafanikio ya Carson katika vipindi vya redio.

Kifo hariri

Carson aliugua ugonjwa wa saratani ya matiti na ugonjwa wa pumu Januari 1964. Hali yake ikawa mbaya zaidi, na mwezi Februari, madaktari waligundua kuwa alikuwa na anemia kali kutokana na matibabu yake ya mionzi, na mwezi Machi waligundua kuwa saratani ilikuwa imefikia ini lake.

Carson alikufa kutokana na saratani 14 Aprili 1964, nyumbani mwake huko Silver Spring, Maryland.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rachel Carson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.