Rafael Alvira
Rafael Alvira (24 Oktoba 1942 – 4 Februari 2024) alikuwa mwanafalsafa wa Kihispania. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Wasifu
haririRafael Alvira alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1942 katika jiji la Madrid. Akiwa na umri wa miaka kumi na minane, alianza masomo yake ya Falsafa katika Chuo Kikuu cha Navarra na kupata shahada za uzamivu (udaktari) katika Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana kilichoko Roma. Alifanya masomo ya ziada katika nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Ujerumani (miaka miwili katika Chuo Kikuu cha Münster), Italia (miaka miwili katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran), Austria, Ufaransa, na Marekani.[1]
Marejeo
hariri- ↑ "Rafael Alvira Domínguez – Ediciones Universidad de Navarra". www.eunsa.es (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2024-03-11.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |