Raimundi wa Penyafort

Raimundi wa Penyafort, O.P., (kwa Kikatalunya Sant Ramon de Penyafort; kwa Kihispania San Raimundo de Peñafort, Vilafranca del Penedès, Catalonia, 1175 hivi; Barcelona, 6 Januari 1275) alikuwa padri maarufu kwa utaalamu wake katika masuala ya sheria.

Mt. Raimundi.
Kitabu chake kimojawapo.
Kaburi lake katika kanisa kuu la Barcelona.

Mkusanyo wake wa sheria za Kanisa Katoliki uliendelea kuwa wa msingi hata karne ya 20. Pia aliandika vizuri sana kuhusu sakramenti ya kitubio[1].

Aliongoza shirika la Wahubiri na kulipatia katiba mpya; pia alisaidia kuanzisha lile la Wamersedari.

Papa Paulo III alimtangaza mwenye heri mwaka 1542 na Papa Klementi VIII kuwa mtakatifu tarehe 29 Aprili 1601.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Januari[2][3].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Martyrologium Romanum
  2. "Calendarium Romanum" (Libreria Editrice Vaticana, 1969), pp. 85 and 114
  3. Martyrologium Romanum

MarejeoEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.