Rais wa Nigeria
Rais wa Nigeria ni mkuu wa dola wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria na kiongozi wa serikali. Vyeo vyake ni "Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria" na Amiri Jeshi Mkuu wa jeshi la Nigeria. Rais wa sasa ni Bola Tinubu.
Masharti
haririKila mtu anaweza kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria kama
- yeye ni raia wa Nigeria
- umri wake ni miaka 40 au zaidi
- ni mwanachama wa chama cha kisiasa nchini na kukubaliwa na chama hiki
Kufuatana na katiba anaweza kuhudumia awamu mbili za miaka minne akichaguliwa tena baada ya awamu ya kwanza.
Madaraka ya rais wa Nigeria
haririKufuatana na katiba rais huwa na madaraka yafuatayo:
- kukubali na kutia sahihi sheria zilizopitishwa bungeni
- kurudisha sheria bungeni akiwa na mashaka kama sheria inalingana na katiba
- kupeleka sheria mbele ya mahakama kuu itakayoamua kama inalingana na katiba
- kuitisha bunge kwa makao maalumu kwa shughuli za pekee
- kusimamika maafisa kufuatana na katiba au sheria
- kusimamika kamati za utafiti
- kuitisha kura ya wananchi kulingana na sheria
- kupokea na kutambua mabalozi wa nchi za nje
- kusimamika mabalozi
- kusamehe wakosaji waliohukumiwa na mahakama
Orodha ya wakuu wa dola na maraisi wa Nigeria
haririKatika orodha ifuatayo kuna majina ya watu waliokuwa wakuu wa dola nchini Nigeria tangu uhuru katika mwaka 1960: