Rakisi (kundinyota)
Rakisi (kwa Kilatini na Kiingereza Hercules) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu.
Jina
haririRakisi ni jina lililotumiwa tangu zamani na mabaharia Waswahili waliojua njia yao baharini wakati wa usiku wakiangalia nyota[2]. Jina hili waliwahi kupokea kutoka kwa Waarabu walioiita الرقيس ar-raqiis linalomaanisha "mchezaji". Katika umbo la nyota watu wa kale walimwona mtu anayepiga goti moja au mtu anayechezacheza. Eratosthenes wa Aleksandria alikuwa wa kwanza aliyemtaja kwa jina la mshujaa Herakles wa mitholojia ya Kigiriki[3] lakini ilichukua muda mrefu hadi jina hili lilishinda majina mengine na hivyo aliitwa Hercules kwa Kilatini.
Hercules ilikuwa moja ya makundinyota 48 zilizoorodheshwa na Klaudio Ptolemaio kwa jina la εν γόνασιν en gonasin yaani "mwenye kupiga goti". Ilipokelewa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia katika orodha ya makundinyota 88 za kisasa iliyotolewa mwaka 1930. [4] Kifupi rasmi ni ‘Her’.[5]
Waarabu waliotafsiri orodha ya Ptolemaio waliendelea kumwita ama الجاثي al-jathi "mpiga goti" au رقيس raqis "mchezaji" na hivyo "Rakisi" ilifika kwa mabaharia Waswahili.
Mahali pake
haririRakisi - Hercules lipo karibu na nyota angavu ya Vega.
Inapakana na makundinyota jirani za Tinini (Draco), Bakari (Bootes), Kasi ya Masakini (Corona Borealis), Hayya (Serpens), Hawaa (Ophiuchus), Ukabu (Aquila),, i ( Sagitta), . Mbweha ( Vulpecula) na Kinubi (Lyra).
Rakisi - Hercules anakaa juu ya Tinini (Draco) akishindana naye katika hadithi ya mitholojia.
Nyota
haririRakisi - Hercules ni kundinyota kubwa leyenye nyota nyingi lakini si angavu sana.
β Beta Herculis au “Kornephoros" ni nyota angavu zaidi. Ina mwangaza unaoonekana wa 2.77 ikuwa na umbali unaokadiriwa kuwa miakanuru 148[6].
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miakanuru) |
Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
β | 27 | Beta Herculis au Kornephoros | 2,78m | 148 | G8 III |
ζ | 40 | 2,81m | 35 | G0 IV | |
α | 64 | Ras Algethi | 3,1 bis 3,7m | 384 | M5 Ib |
δ | 65 | Delta Herculis au Sarin | 3,12m | 79 | A3 IV |
π | 67 | 3,16m | 367 | K2 III | |
μ | 86 | 3,42m | 27 | G5 IV | |
η | 44 | Sophian | 3,48m | 112 | G8 III |
ξ | 92 | 3,70m | 135 | G9 III | |
γ | 20 | 3,74m | 193 | A9 III | |
ι | 85 | 3,82m | 494 | B3 IV | |
ο | 103 | 3,84m | 347 | B9 V | |
θ | 91 | 3,86m | 759 | ||
τ | 22 | 3,91m | 314 | B5 IV | |
ρ | 75 | 4,1m | 403 | A0 + A0 | |
110 | 4,19m | ||||
σ | 35 | 4,20m | 314 | B9 V | |
φ | 11 | 4,23m | 204 | ||
95 | 4,3m | 418 | A5 + G8 |
Tanbihi
hariri- ↑ Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Hercules" katika lugha ya Kilatini ni "Herculis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Herculis, nk.
- ↑ ling. Knappert 1993
- ↑ ling. Allen 1899: Star-Names and their Meanings
- ↑ The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Oktoba 2017
- ↑ "The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ KORNEPHOROS (Beta Herculis), tovuti ya Prof. Jim Kaler, iliangaliwa Oktoba 2017
Viungo vya Nje
hariri- Constellation Guide: Hercules constellation
- Hercules, "Stars", kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
- Star Tales – Hercules, tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Oktoba 2017
- The Deep Photographic Guide to the Constellations: Hercules
Marejeo
hariri- Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 238 ff (online hapa kwenye archive.org)
- Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331