Remigius wa Rouen
Remigius au Remedius wa Rouen (alifariki 771) alikuwa mwanaharamu wa Karolo Nyundo, waziri mkuu wa Wafaranki akawa askofu mkuu wa Rouen, leo nchini Ufaransa, kuanzia mwaka 755. Ndugu wa mfalme Pipino, alifanya bidii ili Zaburi ziimbwe kwa kufuata desturi ya Kanisa la Roma na alichangia sana kueneza liturujia ya Roma badala ya ile asili ya Galia.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari[1].
Tazama pia
haririTanbihi
haririVyanzo
hariri- Genealogie der Franken (German)
- Saint of the Day, January 19: Remigius of Rouen Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine. at SaintPatrickDC.org
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |