Wafaranki walikuwa Wagermanik waliovamia Dola la Roma na hatimaye kujitokeza kama kabila lenye nguvu kuliko yote ya aina hiyo.

Mahali pa Wafaranki katika karne ya 3.
Kazi bora ya usanii majengo wa Kikarolo: kanisa palatina huko Aachen, Ujerumani.
Milki ya Wafranki wakati wa kifo cha Karolo Mkuu mnamo mwaka 814.

Nchi ya Ufaransa imepata jina lake kutoka kwao, ambao waliitawala na kutoka huko wakaeneza himaya yao juu ya sehemu kubwa ya Ulaya Magharibi, wakizuia Waislamu wasiweze kutoka Hispania.

Ushirikiano wao na Mapapa, kama kabila la kwanza la Kijerumani kuingia Kanisa Katoliki bila kupitia kwanza Uario, ni kati ya mambo yaliyoathiri zaidi historia ya Ulaya.

Kilele cha ustawi wao kilifikiwa chini ya mfalme Karolo Mkuu aliyetawala sehemu kubwa za Ufaransa, Ujerumani, Italia ya kaskazini pamoja na Ubelgiji na Uholanzi ya leo. Papa Leo III alimpa taji la Kaizari wa Roma tarehe 25 Desemba 800. Ndio mwanzo wa Dola Takatifu la Roma. Baada ya Karolo milki yake iligawiwa pande mbili zilizoendelea tofauti na kuwa asili ya mataifa ya Ufaransa na Ujerumani.

Marejeo

hariri

Vyanzo

hariri
  • Fredegar
    • Fredegarius (1981) [1960]. Fredegarii chronicorum liber quartus cum continuationibus (kwa Latin na English opposite). Westport, Conn: Greenwood Press. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)CS1 maint: unrecognized language (link)
    • Unknown (1973). Liber Historiae Francorum. Coronado Press. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
    • Woodruff, Jane Ellen (1987). The Historia Epitomata (third book) of the Chronicle of Fredegar: an annotated translation and historical analysis of interpolated material. Thesis (Ph. D.). Lincoln: University of Nebraska. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)

Marejeo mengine

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wafaranki kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.