Ripsime na wenzake

Ripsime na wenzake, akiwemo Gayana (walifariki Etchmiadzin, Armenia, 290 hivi) walikuwa mabikira waliofia Ukristo, wa kwanza katika nchi hiyo[1].

Kaburi la Mt. Ripsime kanisani.

Inasemekana walikuwa wamehama Roma ili kumsaidia Ripsime asiolewe na kaisari Dioklesyano aliyevutiwa na uzuri wake mkubwa.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 29 Septemba[2] au tarehe nyingine kadiri ya madhehebu.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Catholic Online. "St. Rhipsime - Saints & Angels - Catholic Online". Catholic.org. Iliwekwa mnamo 2012-09-23. 
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.